Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Muhogo

Muhogo

Muhogo ni kichaka chenye mbao kinachomea kwa miaka mingi na kina mzizi unaoliwa na humea katika nchi zilizoko kwenye tropiki na zilizo karibu na tropiki duniani.

Pia huitwa yuca, manioc na mandioca. Muhogo una uwezo wa kumea katika ardhi isiyo na rutuba ambapo nafaka na mazao mengine hayamei vizuri; unaweza kuhimili ukame na kumea katika udongo wenye virutubishi vichache. Kwa sababu mizizi ya mihogo inaweza kuhifadhiwa chini ya ardhi kwa mda wa hadi miezi 24, na aina zingine hadi miezi 36 uvunaji unaweza kucheleweshwa hadi soko,utengenezaji na hali zingine zinafaa.

Barani Afrika muhogo hutoa nguvu ya msingi ya kila siku katika lishe. Mizizi hutengenezwa aina tofauti za chembe ndogo, mchanganyiko laini wa unga na maji,unga na kadhalika, ama huliwa baada ya kuchemshwa ama ukiwa mbichi. Katika mingi za nchi zinazokuza muhogo barani Afrika majani pia huliwa kama mboga za kijani zinazotoa protini na vitamini A na B.

Katika nchi zilizoko Kusini mashariki ya bara la Asia na nchi za Marekani ya Latin,muhogo umechukua nafasi ya kiuchumi. Wanga wa muhogo hutumiwa kama kitu cha kuunganisha katika utengenezaji wa makaratasi na nguo na pia hutumiwa kama monosodium glutamate ambacho ni kiungo muhimu cha kulea ladha katika upishi wa huko Asia. Barani Afrika muhogo umeanza kutumiwa kama mbadala mdogo wa unga wa ngano.
 

1
Average: 1 (1 vote)
Your rating: None