Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Msichana kujijengea taadhima

Kujenga taadhima (hali ya kujiamini) kwa mtoto wako wa kike kunaweza kumsaidia kushinda vikwazo na kufaulu katika maisha. Hatua ya kwanza inayolenga kujenga taadhima yake ni wewe mwenyewe. Unaweza kupongeza uwezo wake na kumuhimiza kuendelea kujaribu. Kwa kuwapeleka shuleni unaweza kuwaruhusu watoto wako wa kike kujaribu maarifa yao na kujifunza. Hata ikiwa ataanguka mara kadhaa, hili humsaidia kufahamu ya kwamba anaweza kufanya kila kitu yeye mwenyewe na upendo na usaidizi wako. Ikiwa mara kwa mara unajaribu kuwalinda watoto wako wa kike dhidi ya kila kitu, watakua huku wakijihisi ya kwamba hawana uwezo wa kufanya jambo lolote.
 
Pamoja na sifa kutoka kwako, ikiwa mtoto wako wa kike huenda shuleni, anaweza kupata sifa kutoka kwa waalimu wake na wanafunzi wenzake kwa sababu ya maarifa na mawazo yake. Mtoto wako wa kike atahisi mapenzi yako ukiwa unamthamini vya kutosha na kumpeleka shuleni pamoja na kaka zake. Mara kwa mara zawadi hii hurudishwa kwako kupitia uaminifu.
 
Kujenga taadhima kunaweza kuwaepusha wasichana dhidi ya kutegemea madawa ya kulevya,matatizo ya kula na mienendo mingine yenye madhara.
0
No votes yet
Your rating: None