Mtu anapoambukizwa ugonjwa wa kaswende, mwanzoni huwa haonyeshi dalili zozote. Baada ya wiki mbili atapata kidonda ambacho hakina uchungu katika sehemu nyeti. Kwa sababu kidonda huwa hakina uchungu, watu wengi hawatakibaini kwa urahisi na kitapotea baada ya majuma 4-6.
Mara nyingine baada ya kidonda, kaswende huingia kwenye msururu wa damu na huleta homa, kuumwa na mwili na vidonda kwenye mdomo na sehemu nyeti. Wakati huu, mtu huwa na bakteria nyingi kwenye damu na anaweza kumuambukiza mtu mwingine kwa urahisi ikiwa watashiriki ngono. Ikiwa watu hawa hawatatibiwa, kaswende itabakia mwilini na inaweza kuleta matatizo kwenye ubongo ama kwenye moyo baada ya miaka kadhaa.
Kaswende inaweza kutibiwa kwa kutumia kiua vijasumu au Antibiotics kwa Kiingereza. Matibabu haya huua bakteria zinazosababisha kaswende. Ni muhimu kumaliza kiwango chako chote cha dawa ili kuhakikisha ya kwamba umepona vizuri. Ikiwa mama mja mzito ameambukizwa kisonono, mtoto ambaye hajazaliwa anaweza pia kuambukizwa. Wanawake wote waja wazito hupimwa ikiwa wana kisonono katika kliniki ili watibiwe mapema na kumlinda mtoto dhidi ya kuambukizwa.
Je mwenye kaswende ana HIV vilevile?hao bakteria wanasababishwa na nini?
Asante Liberatus kwa swali lako. Hapana, mwenye kaswende sio lazima awe na virusi vya HIV. Lakini utafiti umeonyesha kwamba, walio na magonjwa ya zinaa kama kaswende na kisonono wamo hatarini ya kuambukizwa HIV. Hii ni kwa sasabu vidonda vinavyosababishwa na magonjwa ya zinaa hurahisisha viini ya Ukimwi kuingia mwilini haraka. Mtu anaambukizwa bakteria za kaswende anaposhiriki ngono bila kinga na mtu ambaye tayari anahuo ugonjwa.
inabidi kutumia kondumu.
jina la kaswende kwa kiingereza linaitwaje?
Saimoni asante kwa swali lako. Kwa Kiingereza, ugonjwa wa kaswende unajulikana kama syphillis. Ili kujikinga kutokana na magonjwa yote ya zinaa ni muhimu kujizuia kwa kutumia mbinu inayojulikana kwa kiingereza ABC of Safe Sex. Mbinu ya kwanza ni kujifunga kufanya mapenzi kamwe mpaka utakapoolewa au kuoa. Mbinu ya pili ni kuwa na mpenzi mmoja na nyote wawili muwe munaaminiana. Mbinu ya tatu ni kutumia kondomu kila wakati unapofanya mapenzi. Ndio Saimoni, KONDOMU ni muhimu sana katika kuzuia magonjwa ya zinaa iwapo unaitumia vilivyo na kwa wakati wote unafanya mapenzi.