Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kuchomeka kwa miale ya jua

Ni raha kuota jua, lakini unaweza kuunguza ngozi yako au kupata saratani ya ngozi.

Kila mara jikinge na “SPF”15 au zaidi unapokuwa nje,hata wakati wa baridi au kukiwa na mawingu.Usiote jua sana kati ya saa 4 hadi saa 9 mchana,wakati huu miale ya jua huwa mikali na kuunguwa ni rahisi.

Ukichomwa kwa miale ya jua, unaweza kujitibu nyumbani.

  • Baada ya kuoga jipake mafuta ya (aloe-vera).Itasaidia kuponya.
  • Ukihisimaumivu, meza aspirini na ujipake mafuta yaliyo na benzini, (benzolaine)’ “Camphor,” au “menthol”.Tazama kiambato kwenye mafuta au uliza mfamasi akusaidie.
  • Weka pamba au kitambaa chenye unyevu ulipoungua.
  • Funika sehemu iliyounguwa kwa kitambaa unapoenda nje.

Muone daktari kwa meraha mabaya ya miale ya jua kasha:

  • Unahisi kichefuchefu, kizunguzungu na una homa.
  • Una lengelenge.
  • Una vipele au ngozi inageuka rangi ya zambarau.
  • Majeraha yanatapakaa kote mwilini kesho yake.
0
No votes yet
Your rating: None