Makamasi yanapojaa puani kutokana na mafua au mzio, kufunguka kwa mifupa ya uso wako unaweza kuhisi kuwa kuna msukumo mkubwa wa nguvu usoni mwako ilihali si vyo .Unaweza pia kusikia uchungu iwapo utaamua kushika mashavu yako au hata popote karibu na pua. Unaweza kutokwa na makamasi ya kijani au kimanjano ambayo huenda yasinuke vizuri, kidonda kooni, kukohoa kupata shida sana unapopumua na kuhisi baridi.
Iwapo mapindi si mabaya sana, unaweza kujihudumia nyumbani.
- Meza vidonge vya kuyayusha makamasi vilivyo na dawa ya “pseudoephedrine” ndani yake.Vidonge hivi vitamaliza kabisa mapindi na utapumua bila shida.Unaweza pia kutumia dawa ya kupulizia mapua kukabiliana na hali hii.
- Unaweza pia kupumua mvuke wa moto au maji moto ili mapua yafunguke.
- Unaweza kumeza dawa za kupunguza maumivu, kuweka kitambaa moto usoni kupunguza uchungu.
- Kunywa vinywaji moto kama chai, maji moto yaliyo na ndimu isiwe kahawa kwani itafanya mapindi yaume zaidi.
- Penga pua lako kwa utaratibu
- Viungo kama tagawizi na kitunguu saumu vinaweza kumaliza kabisa mapindi.
Unahitaji kumuona daktari ikiwa:
- Unatokwa na makamasi ya kijani au kimanjano
- Homa yako isipopoa baada ya juma moja
- Una uvimbe na maumivu kandokando ya jicho lako
- Una maumivu makali ya kichwa na hata baada ya kumeza dawa ya Tylenol au aspirin hayaishi.
- Una joto zaidi ya nyusi 38oc
- Huoni vizuri
- Unajihudumia nyumbani lakini baada ya siku tatu huoni mabadiliko.