Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Polio

Polio ni nini?
Polio ni ugonjwa unaosambazwa na kirusi kiitwacho Polio Virus. Polio virus huishi tu katika binadamu na huingia katika mazingira kwa kusambazwa kupitia kinyesi cha mtu aliyeathirika. Kirusi hiki hupitia njia ya kinyesi hadi mdomoni, haswa katika maeneo yenye usafi duni.
 
kirusi cha Polio pia kinaweza kusambazwa kupitia maji ama chakula kilichonajisiwa – kuna ushahidi ya kwamba nzi pia wanaweza kusambaza kirusi hiki hadi kwenye chakula – ama kupitia mgusano wa moja kwa moja. Ugonjwa huu husambazwa kwa urahisi sana kwa hivyo kuna uwezekano wa mtu yeyote anayeishi na mtu aliyeathirika kuathirika pia. Ingawaje watu wanaobeba kirusi hiki huweza kukisambaza kwa urahisi siku saba hadi 10 kabla na baada ya dalili kutokea, wanaweza kusambaza kirusi hiki kwa majuma mengi kupitia kinyesi.
 
Pindi tu kirusi cha polio virus kinavamia mwili, huzaana katika koo na matumbo na kisha husafiri hadi kwenye neva zako kupitia damu ama limfu. Kinavyosonga katika ufumwele wa neva, kirusi hiki huharibu nyuroni mwendo ambazo hubeba habari baina ya ubongo na misuli yako.

0
No votes yet
Your rating: None