Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Dawa za Kuandikiwa na Daktari

Dawa Za Kuandikiwa Ni Zipi?

Ni zile dawa unazoweza baada ya kuandikiwa na daktari kuwa zinakufaa. Unapomuona daktari, hakikisha kuwa umedadisi na kujua hasa kinachokufanya uwe mgonjwa. Daktari atabainisha dawa inayokufaa zaidi kukabiliana na ugonjwa wako. Atakuandikia kijikaratasi utaenda kwenye duka maalum la kuuzia dawa na utanunua hizo dawa.

 
Mara nyingi, dawa za kuandikiwa na daktari huwa na nguvu zaidi kuliko zile za kununua dukani. Hivyo basi ni muhimu uwe mwangalifu sana unapozitumia. Huwa zina ilani za kukutahadharisha na ni muhimu uzizingatie k.m. kumeza dawa baada ya kula au wakati unapokula ama hata hujala chochote. Pia zina ilani kuhusu madhara mengine yanayoweza kutokea mtu anapomeza dawa hizi k.m. kuhisi kulala, kizunguzungu, kukosa usingizi, kutokwa upele ama kuumwa na kichwa.
 
Dawa za kuandikiwa na daktari zinaweza kuwa ghali iwapo mtu hana mpango wa kimatibabu mahali pake pa kazi. Mtu anaweza kuchukua bima ya matibabu au ajiunge na kampuni ya bima. Katika mpango huu, kampuni huwa inamlipia asilimia fulani kisha humkata polepole kutoka kwa mchango wake, viwango fulani vya pesa huwa vimewekwa. Vikipita, kampuni ya bima huwa imejitolea kugharimia hasa kwa kiwango fulani hata kulipia gharama yote.

 

1
Average: 1 (1 vote)
Your rating: None