Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Uchaguzi wa mbegu za mahindi

Uhifadhi wa mbegu nchini 
Kwa karne nyingi wakulima kote ulimwenguni huchagua na kuhifadhi mbegu za kupanda msimu unaofuatia.Wamefanyia mimea yao uchavushaji mtambuka kwa kutumia mikono au kwa kukuza mimea aina tofauti katika shamba moja ili kuendeleza na kubadilika mimea yao kulingana na hali ya mazingira.
 
Manufaa ya kuhifadhi mbegu za humu nchini
  • Mimea hii ambayo imezoea mazingira ya humu nchini huweza kuhimili mabadiliko ya hali za ukuaji.
  • Aina zingine zinaweza kuwa na uhimili kwa baadhi ya wadudu waharibifu.
  • Zingine zinaweza kuhimili udongo wenye chumvi ama huhitaji maji kidogo.
  • Aina zingine zinaweza kupandwa na kuvunwa mapema ama baadaye katika msimu.
  • Zingine zinaweza kutoa matunda yenye ladha tamu ama nafaka ambazo ni rahisi kupika. 
Wakati wakulima wanatumia mbegu zao wenyewe wana uwezo wa kuendeleza mchanganyiko wa mimea ambayo inafaa matumizi yao wenyewe. Kilimo cha organic farming hufanya kazi vizuri ikiwa mkulima atapanda mimea ambayo itakabiliana na hali ya mazingira yake. Kuhifadhi mbegu na kuzalisha mimea ambayo imezoea hali ya humu nchini ni shughuli muhimu katika kilimo cha organic farming ili kuzalisha mimea ambayo inaweza kuhimili hali ya mazingira yako. 
 
Vianzo vikuu vya mbegu
 
Katika jamii za mashambani,chanzo kikuu cha mbegu ni:
 
Wakulima wa mashamba na buustani
Kwa vizazi vingi, kote ulimwenguni, wakulima wamehifadhi mbegu za mazao yao kwa nia ya kupanda, kubadilishana au kuuza.
 
Benki za mbegu katika jamii na taasisi zingine za jamii humu nchini
Sehemu zingine zina benki za mbegu katika jamii au taasisi katika ambazo hukusanya, kupanda na kuhifadhi mbegu ili kuzisambaza kwa wakulima.
 
Hata kikundi kidogo cha watu kinaweza kuanzisha benki ya mbegu kuhifadhi mbegu na mazao ya sehemu hiyo ili wakulima wayatumie.
 
 
Benki za mbegu za kitaifa na kimataifa
Mashirika ya kitaifa, ya kiserikali na ya kimataifa hukusanya na kuhifahi mbegu kutoka kwa aina tofauti za mimea. Hii huendelezwa kwa ‘kupanda’ kila baada yamiaka michache.
 
Ingawaje benki kubwa za mbegu zinaweza kuhifadhi aina nyingi tofauti za mbegu, haziwezi kuhifadhi aina zote za mbegu za sehemu hiyo ama kubadili aina za mbegu zinazokabiliana na mabadiliko yanayowakumba wakulima wa eneo fulani.  
 
Kampuni za mbegu
Kampuni za mbegu hutengeneza na kuuza mbegu za mimea tofauti tofauti. Kampuni za kibiashara za mbegu kwa kawaida huchagua mbegu zenya mavuno ya juu, ubora na uhimili wa wadudu waharibifu na magonjwa.
 
Hata hivyo kampuni za mbegu haziwezi kuchagua mbegu za mimea ambayo inaweza kunea vizuri katika hali mahsusi za eneo fulani nchini. Aina zingine zinaozouzwa huhitaji pembejeo kama viua wadudu vya kemikali, mbolea na kiwango kikubwa cha maji. Kampuni nyingi za mbegu huzalisha mbegu za aina ya F1 hybrid. Mbegu hizi huzalishwa kwa kuzalisha mtambuka aina mbili tofauti na kuchanganya tabia zao. Kizazi cha kwanza cha mimka kutoka kwa mbegu mahuluti huwa na tabia zinazotamaniwa lakini sio jambo zuri kuhifadhi mbegu hizi kwa sababu tabia hizi hazitapitishwa hadi kwa kizazi kinachofuatia. Kwa hivyo wakulima wanaotumia mbegu mahuluti wanalazimishwa kununua mbegu mpya kila mwaka. Tatizo kuu lingine na uzalishaji wa mbegu za mahindi mahuluti ni ongezeko la ugonjwa unaoitwa madoa ya kijivu kwenye jani (grey leaf spot). Ingawaje wakulima wakubwa wanaweza kununua mbegu kila mwaka, hili haliwezekani kwa wakulima wadogo. Na kwa kuongezea, watu wengi duniani kote hivi sasa wamegundua jinsi ilivyo muhimu kwa mkulima kuendeleza aina mbalimbali ya mimea ya eneo lao.
 
Jinsi wakulima huzalisha mbegu zao wenyewe
Uzalishaji wa mbegu unaosimamiwa na mkulima wa kawaida hujumuisha hatua zifuatazo.
  1. Wakulima hupalilia mimea yao kwa kutumia mikono ili kutoa mimea iliyogonjeka ama sio ya ile aina inayohitajika. Uchaguzi hufanyika kulingana na tabia kwa kujumulisha mavuno ya juu, pembejeo kidogo (ukijumululisha kazi) mahitaji, uhimiili wa wadudu waharibifu na magonjwa, utengenezaji, upikaji na ubora wa ladha, uhifadhi na mapato mazuri ya jumla yote ya viumbe hai katika eneo ambao sio wa nafaka (majani na mashina)
  2. Mimea huvunwa kwa kutumia mikono,hili huzuia uharibifu wa mbegu na kuingiliwa na mbegu za magugu na nyenzo zingine zisizo na hisia.
  3. Baada ya kuvuna, zao hupukutwa na kuoshwa kwa mikono ili kupunguza uharibifu na kunajisiwa, na kisha hukaushwa kwenye jua kupunguza kiwango cha unyevu.
  4. Mbegu kwa kawaida huhifadhiwa kando na nafaka.Mbegu kwa kawaida huning’inizwa juu katika sehemu yenye moshi kama jikoni, ili kupunguza uharibifu unaoletwa na wadudu na, kupunguza kiwango cha unyevu. Pia mbegu zinaweza kuhifadhiwa kwa kuongeza viua wadudu kutoka eneo hilo na /ama viua kuvu (majani ya mkalitusi, mchanga, jivu, mwarubaini) kabla ya kuwekwa katika masunduku maalum na kuhifadhiwa juu ya meko.
 
 
0
No votes yet
Your rating: None

I found your this post while searching for some related information on blog search...Its a good post..keep posting and update the information.
extreme funny picture galleries

»

A thoughtful insight and ideas I will use on my blog. You have obviously spent a lot of time on this. Well done!

small usb flash drive

»

Positive site, where did u come up with the information on this posting? I'm pleased I discovered it though, ill be checking back soon to find out what additional posts you include.
nashville advertising agencies

»