Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Jinsi nyingine za kudhibiti kifafa

Kando na madawa, ni nini kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?
 
Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata amedhibitiwa na matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8 ilhali mtoto anahitaji angalau masaa 9) kunaweza kusababisha mshtuko wa kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia kusababisha shambulizi. Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya kutokea kwa mshtuko wa kifafa. Taa zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa katika watu wengine. Kupumua kwa nguvu wakati unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara katika watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa unaweza kuepuka haya, unaweza kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.
 
2.6
Average: 2.6 (5 votes)
Your rating: None