Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ni wapi naweza kuenda ikiwa sitapata usaidizi?

Kuzirai ambako hakuwezi kudhibitiwa kunaweza kuwa hatari kwa mgonjwa.Huwa hakuwezi kubashiriwa na unaweza kufanyika wakati mgonjwa yuko karibu na moto, anaendesha gari ana jaribu kuvuka barabara, anaogelea ama anafanya kazi akiwa juu (k.m juu ya paa la nyumba). Katika hali hii, kuzirai kutamweka mtu katika hatari kubwa kwani anaweza kuchomeka, kupatwa na ajali, kuzama ama kuanguka na kuumia. Hii ni sababu moja muhimu ambayo inahitaji kifafa kudhibitiwa.
 
Pili, ugonjwa wa kifafa unaweza kutokea mara kwa mara ukiwa hautadhibitiwa. Kuzimia kunaweza kutokea mara kwa mara na kuonekana ni kama unaendelea. Hii ni dharura ya kimatibabu ambayo inaweza kusababisha kifo katika mda mfupi. Kwa hivyo ikiwa mgonjwa ataathiriwa na kifafa kwa zaidi ya dakika 5, mpeleke katika hospitali iliyo karibu haraka iwezekanavyo kwa sababu kuzimia hakuwezi kuisha bila ya dawa.
0
No votes yet
Your rating: None