Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kwa nini wagonjwa wa kifafa hawawezi kugawana madawa yao?

Madawa ya kifafa hufanya kazi ya kukomesha shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo. Kuna aina nyingi za kuzirai katika kifafa na hizi zote huitikia kwa njia tofauti kwa madawa tofauti. Hii ndio sababu ya kwanza kwa nini haufai kugawa dawa za kifafa. Dawa ambazo hudhibiti aina moja ya kifafa zinaweza kukosa athari kwa aina nyingine ya kifafa.
 
Pili, watu tofauti wanahitaji vipimo tofauti vya dawa iliyotolewa kudhibiti kifafa. Ugonjwa wa kifafa unamaanisha ya kwamba ubongo wa mtu unaweza kufyatuka kwa njia isiyo ya kawaida. Watu tofauti hupata kifafa katika viwango tofauti vya mchangamsho wa ubongo. Watu wengine huchangamshwa kwa urahisi na kuzirai ilhali wengine hawachangamshwi kwa urahisi. Kipimo cha dawa kinachotumiwa kumdhibiti mtu ambaye huzirai kwa urahisi ni tofauti na kile cha yule ambaye hazirai kwa urahisi.
 
Tatu, sio vizuri kugawana madawa ambayo yametolewa kufuatia maagizo ya dakitari. Maagizo ya dakitari hutoa dawa kwa mtu mmoja kwa kipindi maalumu cha wakati. Kwa kugawana madawa, mtu ambaye alipewa maagizo ya dakitari ataishiwa na dawa kabla ya ahadi ya kuonana na dakitari inayofuatia. Wanweza kuzirai kwa urahisi kwa sababu hawako kwenye matibabu. Sio salama kwa mtu mwenye kifafa kugawa dawa zake.
4
Average: 4 (1 vote)
Your rating: None