Siwezi kumbuka ikiwa watoto wangu walipata viwango vyote 4 vya chanjo wakati walipokuwa wachanga, je wanahitaji kuchanjwa mara tena?
Ndiyo. Ikiwa hauna uhakika kama watoto wako walipata VIWANGO VYOTE 4 vya chanjo ya kupooza walipokuwa wachanga, unashauriwa kuwachanja tena.
Viwango 4 hutua kinga 100% dhidi ya ugonjwa huu daima. Hili lina maana ya kwamba ikiwa ulipata viwango vyote 4 vya chanjo ya kupooza, basi umelindwa dhidi ya ambukizo la kupooza katika maisha yako yote.
Kwa hivyo ni muhimu kwa kila mtu katika jamii yako kuchanjwa dhidi ya kupooza na kuhakikisha ya kwamba kila mtu anapata viwango vyote 4 vya chanjo.
Ikiwa watoto wangu watachanjwa watakuwa wagonjwa na hatimaye watakufa?
Hili ni shauku la kawaida kwa wazazi wakati wanapoombwa watoto wao wachanjwe dhidi ya kupooza
Ni muhimu kukumbuka ya kwamba kupooza ni ugonjwa ambao husababishwa na kirusi kwa hivyo hauwezi kutibiwa pindi mtu anapoambukizwa. Hata ikiwa mtu hana dalili za ambukizo, bado anaweza kupitisha ambukizo hili hadi kwa watu wengine, haswa mahali ambapo usafi na udhibiti afya ni mbovu.
Ingawa katika visa vingi, mtu aliyeambukizwa huwa hana dalili zozote, kuna visa ambavyo mtoto ama mtu mzima hupooza kutokana na ambukizo la Polio. Polio ni chanzo muhimu cha kupooza ambako kunaweza kumalizwa kabisa duniani kote kupitia chanjo na kudumisha usafi bora. Kwa hivyo ni muhimu kwa watoto wote na watu wazima duniani kote kuchanjwa dhidi ya polio.
Kuna visa vichache ambavyo baada ya chanjo, mtoto hupata aina isiyo kali ya ugonjwa huu.Jambo hili sio la kawaida na halifai kuwakata watu moyo katika jamii wasifanye kazi ya kumaliza polio kutoka katika jamii.
Mtoto wangu ana zaidi ya miaka 3; je nahitaji kumpeleka apate chanjo wakati wa kampeini za chanjo?
Ndiyo, ni muhimu kwa watoto wote kushiriki katika chanjo wakati wa kampeini.
Polio ni ugonjwa ambao unaweza kuwaathiri watoto wa umri wowote na watu wazima. Ni muhimu kila mtu achanjwe dhidi ya ugonjwa huu. Katika maeneo ambapo udhibiti afya, ukosefu wa maji safi na usafi , ugonjwa wa polio huenea katika jamii.
Chanjo dhidi ya polio ndiyo njia pekee mwafaka ya kupambana na ugonjwa huu na ni lazima tuunge juhudi za KUMALIZA POLIO HIVI SASA!