Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

  • Vidokezi vitano namna ya kujikinga kutokana na homa ya nguruwe

Vidokezi vitano namna ya kujikinga kutokana na homa ya nguruwe

Homa ya nguruwe au H1N1 (jina la technologia la virusi) ni ugonjwa ambao watu wanafaa kuwa makini nao na wachukue hatua za kujikinga pamoja na familia zao ili kudumisha afya bora.

Virusi vya homa hii vinatishia maisha ya kila mtu, vijana, wazee wale ambao tayari wanaugua magonjwa mengine, walio ambukizwa n.k.Ni muhimu kuhakikisha kuwa tumejitunza na kuzuia homa hii kumshika mtu yeyote.

Hebu chukua muda, upitie kwenye kituo cha kutibu na kukabiliana na homa ya nguruwe ama home yoyote ile.Pia itahakikisha kuwa hii homa haienei na kuambukizwa watu kiholela.

  • Keti nyumbani unapokuwa mgonjwa
  • Usiwe na uhusiano wa moja kwa moja na wale ambao tayari wameshikwa na homa hii
  • Nawa mikono kila wakati,epukana kabisa na kushika macho,pua na mdomo
  • Funga mdomo na pua kwa karatasi shazi au kitambaa unapokohoa au unapochemua.
  • Jua ujumbe wote unaohusiana na afya bora katika jamii yako.

Vidokezi hivi unavifahamu? Misingi ya homa ya mafua ni sawa na ile ile ya binadamu na ya nguruwe ni homa inayotatiza hali ya mtu ya kupumua.Husababishwa na vijidudu vimelea vya homa hii ambayo hhutokea mara kwa mara kwa nguruwe .Mara nyingi,watu huwa hawapati homa ya nguruwe bali maambukizi yanayotokana nayo.

Hii homa huenea tu kwa njia moja nay a kawaida, maambukizi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia kwa kukohoa, kuchemua, na kushika mtu aliyeambukizwa au kushika mahali ambapo kuna hivyo virusi.Pia kushika milango vijigari vya kubeba mizigo dukani (trolly) n.k.Hivyo basi ni vyema kujibebea,dawa au sabuni ya kuua vijidudu na uchafu.

Kuna habari njema .Kuna dawa za kuzuia maambukizi ya homa tata na pia homa ya nguruwe.Pia huweza kuzuia shida sugu za homa. Pili virusi vya homa ya nguruwe haviambukizwi kupitia kwa chakula.Hivyo basi hakuna haja ya kukataa nyama ya nguruwe.Vyakula vinavyotokana na nyama ya nguruwe, mradi tu vimetunzwa vizuri, havidhuru.

Sasa iwapo unaishi katika sehemu ambazo homa ya nguruwe imegunduliwa kuwa ipo,zuru kituo cha afya kilicho karibu mradi tu umeona dalili za homa hii.Dalili za homa hii ni joto jingi, kuumwa na viungo vya mwili mafua ,koo kuwasha ,kusikia kichefuchefu, kutapika na kuhara.Mhudumu wako wa kiafya atakupa mwongozo ili ujue iwapo unahitaji kufanyiwa matibabu au majaribio kwanza.

Ikiwa unafuata haya maagizo ya kimsingi kuhusu namna ya kukabiliana na mafua, basi utapunguza uwezekano na kuweka ugonjwa mwilini, pamoja na homa ya nguruwe.

4
Average: 4 (1 vote)
Your rating: None

Is it okay to post part of this on my website basically post a hyperlink to this webpage?
real estate marketing ideas

»