Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Jinsi ya Kusoma Ripoti ya Mkopo (How to Read a Credit Report)

Ripoti ya mkopo inaweza kuonekana kukuchanganya kwa mara ya kwanza, kwa hiyo ni rahisi kuisoma kwa kuipitia na kuigawa katika vifungu vine vya msingi:

  1. Maelezo Binafsi?
  2. Rekodi za Umma
  3. Maelezo ya Akaunti ya Mkopo
  4. Maulizio

1. Maelezo Binafsi

Haya ni maelezo ya kimsingi kama vile anwani yako ya sasa na awali, tarehe ya kuzaliwa, namba za simu, namba za leseni ya kuendesha motakaa, mwajiri wako, na jina la mwenzi wako. Yaangalie kuhakikisha kuwa yako sahihi.

2. Rekodi za Umma

Sehemu hii inaorodhesha matukio kama vile kufilisika, hukumu na madai ya kodi

3. Maelezo ya Akaunti ya Mkopo

Hii ni orodha na maelezo juu ya akaunti zako mbalimbali. Maelezo kuhusu akaunti yanaweza kuwa pamoja na lini ulipofungua akaunti, jumla ya mkopo au kiwango cha juu cha salio kwenye kadi, unadaiwa bado kiasi gani, na jinsi ambavyo umekuwa unalipa
akaunti hiyo. Sehemu hii ni pamoja na akaunti zinazozunguka (credit cards) na akaunti za malipo yaliyopangwa kwa muda (mikopo ya magari, mikopo ya shule au malipo ya nyumba)

4. Maulizio

Hii ni orodha ya kila mtu ambaye ameomba kuona ripoti yako ya mkopo, kukiwa pamoja na wewe mwenyewe. Sehemu hii haiathiri sifa zako za mkopo kama ilivyo historia yako ya ukopaji au rekodi za umma”

Kagua Ofisi za orodha ya Mkopo

Ofisi tofauti zinazoorodhesha ukopaji, Equifax, Trans Union au Experian zitakuwa na maelezo tofauti, na ni kawaida kuwepo makosa katika ripoti za mkopo, kwa hiyo habari zako za ukopaji zitakuwa sahihi zaidi ikiwa utasahihisha makosa ndani ya ofisi zote tatu zinazoorodhesha ukopaji wako

Angalia sampuli kutoka kampuni zote tatu zinazoripoti ukopaji wako:

  • Chunguza Ripopti ya Mkopo ya Equifax
  • Chunguza Ripoti ya Mkopo ya Experian
  • Chunguza Ripoti ya Mkopo ya Trans Union


(Personal Information) Maelezo ambayo wewe na wanao mnapaswa kuwa  waangalifu juu yake kwenye mtandao, kama vile namba za simu za mkononi, barua pepe, jina unalotumia kwenye mtandao, jina la ukoo, anwani, na picha.

0
No votes yet
Your rating: None