Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Saratani ya Makodo (Testicular)

Saratani ya makodo au mapumbu ndio inayojulikana sana hasa kwa vijana barubaru wa kati ya miaka 15 hadi 35. Habari njema ni kuwa saratani ya makodo ni haba sana na inatibika.

Licha ya kutoa mbegu za uzazi, makodo pia hutengeza homoni za kiume. Makodo ni laini, mviringo na ngumu. Wanaume wanahitaji kujikagua wenyewe mara kwa mara kila mwezi kutambua mabadiliko.
 
Wanaume wengine wamo hatarini zaidi mwa kupata saratani ya makodo:

  • Watoto wa kiume waliozaliwa na makodo isiyo ning’inia chini.
  • Wanaume ambao makodo yao hayakumea kawaida.
  • Wanaume waliozaliwa na Klinefelter’s Syndrome (Hali ya mvulana kuzaliwa na chromosome zaidi ya 46 iliyo kawaida. Akikua mwili wake una dalili za uke kama vile matiti na kutokuwa na nywele usoni)

Dalili za Saratani ya Makodo

  • Uvimbe usiyo na uchungu kwa kodo
  • Uchungu ndani ya kodo
  • Kodo kuwa ngumu na kubadilika kwa saizi. (Kuvimba au kurudi). Kuhisi uzito kwa mapumbu (mfuko wa makodo)
  • Uchungu usio mkali kwa manena na sehemu ya chini ya tumbo.
  • Matiti kuwa makubwa au kuuma.

Hizi pia zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengine ambayo si saratani. Ukihisi dalili yoyote ya hizi, muone daktari.

 

2.5
Average: 2.5 (4 votes)
Your rating: None

Your website is really cool and this is a great inspiring article. Thank you so much.
linkedin careers

»