Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Saratani ya Nyumba ya Uzazi. (Uterine)


Aina hii ya saratani huwa katika nyumba ya uzazi, pale mtoto anakulia. Kuna aina tofauti ya saratani ya nyumba ya uzazi: Endometrial (Utando unaofunikasehemu ya ndani ya nyumba ya uzazi) na Sarcomas (uvimbe wa saratani katika misuli au mifupa). Endometrial ndio inayojulikana zaidi na huvamia sehemu nyepesi ya nyumba ya uzazi. Sarcomas ambayo ni nadra sana huvamia misuli inayosaidia nyumba ya
uzazi, ni muhimu kumuona daktari kila mwaka kwa uchunguzi.
 
Ni zipi hatari za kuwa na ugonjwa huu?

  • Kuwa na miaka 50 na zaidi.
  • Kutumia madawa yenye hormone
  • Ukiwa na endometrial hyperplasia
  • Uzito wa kupita kiasi
  • Ikiwa umewahi kuwa na saratani ya utumbo mpana (Colorectal)


Ishara zake ni zipi?

  •     Uvujaji wa damu usio wa kawaida kutoka kwa uke
  •     Kuvuja zaidi wakati wa hedhi
  •     Uchungu unapokojoa au kushiriki ngono
  •     Maumivu sehemu ya chini ya tumbo
  •     Damu katika kinyesi au mkojo wako


Ishara hizi zaweza kuwa kitu kingine, lakini muone daktari mara moja ukihisi mojawapo ya dalili hizi.
 
 

 

2.333335
Average: 2.3 (3 votes)
Your rating: None

Wow i can say that this is another great article as expected of this blog.Bookmarked this site..
linkedin careers

»