Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Dutu – Insulin 101

Insulin ni homoni inayotengenezewa katika kongosho (pancreas) zetu. Inaruhusu sukari iliyo katika chakula kuingia kwa seli (cells) na kupatia mwili nguvu za kufanya kazi.  

Mbona watu wanaihitaji?
Kwa watu wanaougua ugonjwa wa Sukari wa aina ya kwanza(1), kongosho zao huwa hazitoi Insulin. Hivyo basi, watahitaji kudungwa na Insulin ili kusaidi mwili kutumia sukari iliyo kwa chakula. Wanaougua aina ya pili (2) ya ugonjwa wa Sukari, kongosho zao zinatoa Insulin lakini sio ya kutosha na haifanyi kazi vizuri. Walio na aina ya pili (2) ya ugonjwa wa Sukari wanameza tembe za kisukari au wanadungwa na Insulin.
 
Ni yapi madhara ya kuwa na kiwango cha chini cha Insulini ama kuikosa kabisa mwilini?
Insulin husaidia mwili kutumia sukari inayopatia mwili nguvu. Bila Insulin, sukari haiwezi kuingia kwa seli (cells) kwa hivyo kiwango cha sukari damuni kinaongezeka. Kiwango cha sukari cha juu katika damu kinaweza sababisha hali zifuatazo: 
  • Kutoona vizuri
  • Kuhisi kiu sana
  • Kuwa mchovu kila mara
  • Kukojoa mara nyingi
  • Kuharibika kwa viungo vya mwili 
Insulin hutumiwaje? 
Haiwezi kumezwa kama tembe lazima udungwe ndani ya mafuta yapatikanayo chini ya ngozi ili iingie ndani ya damu mara moja. Kulingana na chama cha Ugonjwa wa Sukari Cha Amerika kuna zaidi ya aina ishirini (20) za Insulin zinazouzwa.

 

3
Average: 3 (1 vote)
Your rating: None