Huu ni ugonjwa wa zinaa ambao ni wa kawaida na huathiri wanawake na wanaume kwa njia tofauti. Katika wanaume, dalili hutokea baada ya siku 2-5 baada ya kufanya mapenzi. Dalili dhahiri ni utetelezi ama usa mzito wa manjano kutoka kwenye uume. Hili husababisha hali ya kuchomeka na uchungu wakati unapokojoa. Uume unaweza kuwa mwekundu, kuvimba na huhisi uchungu unapoguzwa.Wanaume wachache huwa hawaonyeshi dalili zozote. Ikiwa hautatibiwa, unaweza kuharibu uume na kuzuia kupita kwa mkojo na manii.
Katika wanawake, dalili huwa sio dhahiri. Nusu ya wanawake ambao wameathiriwa na kisonono huwa hawaonyeshi dalili zozote na kwa hivyo huwa hawatibiwi. Wao huzidi kuambukiza watu wengine na mara kwa mara huathirika na matatizo ya vifuko vilivyo jifunga, ugumba na uchungu unaojirudia rudia katika sehemu ya chini ya tumbo (chronic pelvic pain). Wale ambao wana dalili hizi hupata homa, huhisi uchungu wanapokojoa na hutoa usaha kutoka kwenye uke baada ya siku 2-5.
Kisonono hutibiwa kwa urahisi haswa ikiwa matibabu yataanza mapema. Mtu huhitaji tu kutumia kiua vijasumu (antibiotics) kwa siku 7-10 ili apone. Mtoto anayezaliwa na mama ambaye hajatibiwa kisonono anaweza kupata ambukizo hatari la macho wakati wa kuzaliwa. Hili litahitaji matibabu na matone ya macho ya kiua vijasumu (antibiotics).