
Huu ni ugonjwa wa zinaa ulio hatari zaidi kwa binadamu. Unasababishwa na kirusi kinacho sambazwa kwa urahisi wakati unapofanya mapenzi. Pia huambukiza watoto ambao hawajazaliwa wakati wa kuzaliwa na wanaponyonyeshwa. Hakuna tiba ya HIV na hivi sasa zaidi ya watu milioni 30 wameambukizwa kote ulimwenguni. Wengi wa watu walioambukizwa huishi katika nchi za Afrika zilizoko chini ya jangwa la Sahara na Wakenya 500 hufariki kila siku kutokana na Ukimwi.
Virusi huingia mwilini na kuharibu seli za ulinzi katika mwilini (kinga ya mwili). Pindi tu kinga ya mwili imedhoofika, mwili huathirika na maambukizo mengine mengi ambayo husababisha kuharisha, kutapika, kuumwa na kichwa, homa ya uti wa mgongo (menengitis), maambukizi ya ngozi na nimonia na hatimaye mtu asipotibiwa hufariki kutokana na moja ya maambukizi hayo.
Kuna madawa yajulikanayo kama ARV yanayopatikana katika hospitali za wilaya ambazo hupunguza kiwango cha ukuaji wa virusi katika mwili. Madawa haya kwa hivyo yataendeleza afya ya mtu na kurefusha maisha yake. Hata hivyo hii sio tiba na virusi vitabakia mwilini. Mtu aliyeathirika anaweza kumuambukiza mtu mwengine na mbaya zaidi anaweza kujiambukiza tena mara tena. Na kwa kila ambukizo, kinga ya mwili hudhoofika na afya ya mtu hudhoofika.
Unaweza kufanya nini?
nimefurahi sana kusoma katika ukurasa huu nimependa sana kuhusu kujikinga na ukimwi na kuhamasisha,nyuki na bajeti,nimejifunza mambo mengi naendelea kusoma
Bi.Anna
Asante sana kwa kuchukua nafasi na kusoma.Endelea kusoma Beehive na utajua mengi zaidi.Ukiwa na maswali na hoja ungependa kujua zaidi,tujulishe na utapata usaidizi.
Asante sana.
Tuungane sote kuangamiza ukimwi
Habari Bi Pamela,
Asante sana kwa kuchukua nafasi,endelea kusoma zaidi.