Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Je unajua hali yako ya HIV?

Jina langu ni Musa Harun. Mimi ni mwanafunzi katika Chuo cha Teknologia na pia ni kijana anayefunza vijana wenzake kuhusu afya. Kuwa kijana anayewafunza vijana wenzake kunahitaji mtu kuwa mfano mwema na aweze kutoa mwelekeo. Hii ndio sababu nilienda katika kituo cha VCT ili kupimwa ikiwa nina virusi vya HIV. 
Kituo kinachotoa huduma za ushauri na upimaji wa hiari (VCT)
Maono yetu ni kukuza ufahamu wa hali ya HIV kupitia uvumbuzi wa mikakati ya kutoa ushauri na upimaji. Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa katika sehemu ya mapokezi katika kituo cha VCT nilichokitembelea huko Kericho. Kama kijana aliye katika miaka ishirini ya mwanzoni, nilikaa pale, huku nikiwa nakerwa. Ilikuwa kama kwenda katika majaribio ya mambo uliyofanya maishani huku ukiwa hauna dhana yoyote kuhusu matokeo ya uamuzi na jambo hili linaweza kuwa la kuogofya. Nilikuwa hapa kupimwa HIV.
Niliitwa na kuingizwa katika chumba kidogo.Kina meza moja pekee,viti vitatu na vifaa vinavyotumiwa katika upimaji.Mwanadada aliyenikaribisha alinionyesha urafiki na alinisemeza kwa upole. Alikuwa kijana kama mimi na alipoanza kutoa maelezo kuhusu kile kitafanyika, nilihisi naanza kupumzika.
Kabla ya upimaji
‘Kabla ya upimaji, ningependa tuzungumze kidogo kukuhusu na HIV na UKIMWI’. Nilitikisa kichwa na aliendelea kunielezea mambo muhimu kuhusu usambazaji wa HIV na jinsi hukua hadi kufikia UKIMWI. Pia alinieleza jinsi upimaji utafanyika. Alimalizia, `kumbuka ya kwamba mistari miwili inaashiria ya kwamba una VVU, mstari mmoja unaashiria ya kwamba hauna HIV.’
 
Kisha ikafika sehemu iliyokuwa ngumu; ‘‘Ushawahi kushiriki ngono?’’aliniuliza. Niliona aibu. Nilitaka kudanganya lakini nilifahamu hiki kilikuwa kilele cha majaribu. Nilikuwa hapa kujua ukweli kwa hivyo nilihitajika kuwa mkweli. Nilijibu ndiyo, nikiwa na matumaini ya kwamba hataniuliza nilishiriki ngono na nani na mara ngapi. Kwa bahati nzuri kile kilichofuatia hakikuguzia ujinsia wangu. Alinihakakishia ya kwamba kufanyiwa upimaji lilikuwa jambo bora kwani licha ya matokeo; itanisaadia kuchukua hatamu ya maisha yangu.
Upimaji
Kufikia hivi sasa nilijihisi mtulivu.Kisha akaniuliza ikiwa nikuwa tayari kwa upimaji. Nilisema ‘ndiyo’. Alivaa glavu zake na kisha akasafisha kidole changu cha pete na antiseptiki. Kwa kuwa na utambuzi kuwa ni haki na wa kufanya jambo kutokana na miaka 2 ya utendaji kazi, mshauri alidukua kidole changu na kutoa tone la damu na kuliweka kwenye kifaa kinachotumiwa kupimia.
Huku nikiwa nimekodoa macho, nilitazama jinsi vidole vyake viliruka kutoka kwa kitu kimoja hadi kingine katika onyesho ambalo limefanyika zaidi ya mara mia moja kabla yangu. Ilinibidi ningoje dakika 15 ili matokeo yawe tayari. Hizi dakika 15 zilinikulia kama kwamba ni milele na niliteswa kiakili vibaya.
Katika akili yangu, nilianza kujiuliza. Kweli nilikuwa tayari kujua hali yangu? Kwani ilikuwa lazima? Je ikiwa nina HIV? Ndiyo nilikuwa nimepitia ushauri lakini ni kawaida kwa binadamu kuogopa. Nilijaribu kujipa moyo. Maelfu ya watu wamepimwa tangu vituo vya VCT vianzishwe. Baada ya kupiwa watu wengi wameishi na matumaini na na virusi hivi. Nilifahamu ya kwamba mimi niko katika kikundi kinachoshiriki ngono na ambacho kinakisiwa kuwa katika hatari kubwa ya kupata HIV. Kwa hivyo nilisubiri. Mshauri alisubiri nami huku tukiongea polepole. Alikuwa akinipoza.
 
Matokeo
‘‘Nafikiri matokeo yako yako tayari na unaweza kuyatazama.Kumbuka ya kwamba mistari miwilli inaashiria ya kwamba una HIV, mstari mmoja unaashiria ya kwamba hauna HIV,’’ mshauri wa VCT alinieleza. Katika hatua hii miguu yangu ilikuwa ikitetemeka na sikuwa naona vizuri. Mahali ninapotoka sisi husema mtu anapaswa kujitayarisha kufa mara mia moja. Wakati ulikuwa umewadia. Nilipiga moyo konde na nikatupia jicho kifaa kinacho onyesha matokeo ya upimaji - mstari ulikuwa tu mmoja. Ungehisi kushusha pumzi kwangu kwa faraja hata ikiwa ungekuwa nje! Nilikuwa na furaha isiyo na kifani.
Baada ya upimaji
Mshauri alinishauri jinsi ya kubakia bila ya HIV kwa kuzingatia kanuni ama ABC za kuzuia uambukizaji wa HIV na UKIMWI ambazo ni kutoshiriki ngono, kuwa mwaminifu ama kutumia mpira wa kondomu kila unapofanya mapenzi. Lakini bado nilikuwa na swali moja la mwisho, ‘Je ikiwa ningepatikana nina HIV?’ Mshauri alinijibu, ningekupa ushauri wa jinsi ya kusimamia hali yako ya HIV. "Ningekutuma kwa mtu anayetoa huduma ya matibabu ili uanze usimamizi wa HIV".
Nilitoka kwenye chumba hicho nikiwa na furaha, lakini pia nikiwa na jukumu kubwa la kuwashauri marafiki zangu, huku nikiwa na ufahamu ya kwamba kujua hali yako ya HIV kunakupa usimamizi wa maisha yako.
2
Average: 2 (6 votes)
Your rating: None