Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kuishi vyema na HIV na UKIMWI

Ikiwa umetoka kupimwa na umepatikana na VVU, tukio hili linaweza kuwa la kuogofya. Hata hivyo, ni muhimu kufahamu ya kwamba kuwa na HIV hakumaanishi ya kwamba utakuwa mgonjwa mara moja na utafariki hivi karibuni.

Virusi vya HIV vinaweza kudhibitiwa kwa utunzi mwafaka, tiba na kuwa na mafikira mema, mtu anaweza kuishi maisha ya kawaida kama mtu yeyote.

Ni nini kwanza unachofaa kufikiria ama kufanya ikiwa una HIV?

HAUKO PEKEE YAKO

Hii ni kwa sababu:-

  • Kuna watu wengi wenye virusi vya HIV
  • Kuna watu wengi wenye UKIMWI
  • Watu wengi wanasumbuliwa na VVU na UKIMWI

ONGEA NA MTU

Watu wenye HIV na UKIMWI wanahitaji kuongea na mtu kuhusu hali yao ama mafikiria yao. Ni jambo la kuogofya kuwa na HIV ama UKIMWI. Unaweza pata ya kwamba utapunguzia mzigo ikiwa utaongea na mtu anayeelewa.

ISHI KAMA KAWAIDA
Ikiwa una VVU na UKIMWI usikate tamaa.

  • Kuwa msafi na vaa nguo nadhifu
  • Jishughulishe.
  • Fanya kitu kitakachowasaidia watu. Jihusishe na familia na marafiki zako – usijitenge nao – bado wanakuhitaji.

TANGAZA HALI YAKO IJULIKANE

Ikiwa una VVU ama UKIMWI usijifiche. Mwanzoni watu watakuzungumzia lakini usife moyo.

  • Jishughulishe katika jamii. Kwa njia hii, wengine wataanza kukuona kama mwanajamii wa kawaida na mwenye manufaaa katika jamii na wataanza kukuthamini. Inaweza pia kuwapa hima wangine kama wewe na pia inaweza kuwa njia kwako na kwao kujenga kikundi cha kujisaidia.

KUWA NA TAFAKARI NJEMA KUJIHUSU

  • Jivunie. Usiwache kile mtu anasema kikuvunje moyo.
  • Wewe bado ni muhimu. Wewe bado ni wewe. Tembea wima.

Katika sehemu hii, unaweza kupata habari jinsi watu wenye HIV na UKIMWI wanaweza kujilinda na kujitunza na kuwatunza wale walio karibu nao.

3.6
Average: 3.6 (5 votes)
Your rating: None

HIV / Aids is to make a person lose hope no exception obat keputihan gatal

»

Its a great pleasure reading your post.Its full of information I am looking for and I love to post a comment that "The content of your post is awesome" Great work.
thermogenic

»