Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Matibabu Hospitalini

Kuna mambo machache ambayo unatakikana kuyafanya na machache ambayo hutakikani kuyafanya.

  • Nenda kwa kituo cha afya cha umma ama umwone daktari wa kibinafsi aliye mjuzi wa mambo yanayohusiana na ukimwi. Ukishahakikisha kuwa, una muuguzi au daktari unayeweza kumwamini na una uhusiano bora naye, nenda mara kwa mara wakuangalie ili waone vile unavyoendelea kudhibiti maambukizi ya ukimwi.
  • Utahitaji ufanyiwe hesabu ya chembechembe zako za CD4 na wingi wa maambukizi yaliyo mwilini mwako mara mbili kwa mwaka
  • Karibu kila mtu aliye na virusi vya Ukimwi (asili mia 97%) baadaye atapata ugonjwa wa Ukimwi au magonjwa mengine yanayohusishwa na ugonjwa huu. Haya huitwa, magonjwa yanayotumia nafasi hii ya hali iliyoko mwilini kukuangamiza. Karibu magonjwa yote ya aina hii yanaweza kutibika kwa kutumia dawa zilizodhibitishwa.
  • Kwa watu wengi, Ukimwi ni ugonjwa ambao hauwezi kutibiwa hata hivyo, ni hali inayoweza kudhibitiwa kama magonjwa mengine yoyote ya kudumu ambayo hayana tiba. Watabibu wanajua kuna dawa za kudhibiti haya maradhi, (antiretrovirals - ARVs) ya kusaidia watu kuishi maisha ya kawaida na kwa mda mrefu wakiwa na virusi vya ugonjwa huu. Hata hivyo unachohitaji kujua ni kuwa ni muhimu uanze kutumia hizi dawa za ARV za kudhibiti ugonjwa hasa unapo ambukizwa na maambukizi yanayoambatana na magonjwa haya (yanayojulikana kama magonjwa yanayotumia nafasi au hali ya mwili wako ya kuwa umeambukizwa). Ama wakati ambao chembechembe zako za CD4 ni chini 350. Kwa watu wengi walio na virusi vya ukimwi, haya hutokea kwa kati ya miaka 8 – 10 baada ya maambukizi. Hata hivyo kuna hali fulani ambazo hazifuati hali hii.
  • Kuna ushahidi wa kuaminika kuwa ukitumia tembe badala ya vitamini kila siku kidogo unapunguza makali ya ukimwi na haukuporomoshi haraka. Jaribu utumie tembe badala zilizo na vitamini B, C na E. Vituo vya afya vya umma vinafaa kuwapa wagonjwa bure, bila malipo, hizi tembe. Tambua kuwa kuna madai mengi ya uongo kuhusu hizi tembe badala ya vitamini. Haya madai huwa yametiwa chumvi na poroja kali. Haijathibitishwa bado iwapo, mtu anakula virutubishi vyote vya mwili kwa chakula anastahili pia kutumia tembe hizi ili ziwe za manufaa kwake.

 

0
No votes yet
Your rating: None

Positive site, where did u come up with the information on this posting? I'm pleased I discovered it though, ill be checking back soon to find out what additional posts you include.
bearpaw emma

»