Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ihifadhi

Je unapenda kununua chai kila asubuhi? Unavuta sigara? Ni burudani gani umezoea kila siku?

Ukihifadhi kiasi kidogo cha pesa kila siku, hatimaye utakuwa na idadi kubwa. Lengo kuu ni kuanzia na kiasi kidogo.

Zifuatazo ni sababu nzuri zakuhifadhi pesa:

  • Unajiandaa kwa mahitaji ya dharura kama bili ya hospitali au ukarabati wa nyumba au gari.
  • Kukuwezesha kununua bidhaa zenye gharama ya juu kama fanicha, vifaa vya nyumba au kwenda safari ya likizo katika siku za usoni.
  • Mpango wa kustaafu. Unadhani unaweza ukaishi kwa pensheni peke yake? Kuweka pesa za ziada kwa weza kukusaidia kuwa na maisha mema baada ya kustaafu.
  • Kuweza kuwekeza. Pengine huna pesa za kutosha kuwekeza kwa sasa lakini unaweza kuhifadhi kidogo kidogo mpaka itoshe ya kuwekeza. Mipango ya muda mfupi inaweza kubadilika na kuwa ya muda mrefu.