Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Elimu

Ikiwa unataka mtoto wako apate elimu bora, huo ndio wakati wa kuanza kuweka akiba kwa ajili hii!

Hata katika shule ya serikali unaweza kuhitajika kulipa karo. Ongeza hili katika kununua sare za shule, vitabu,vifaa vya kuandikia na kadhalika, na gharama zinalindikizana. Kupata pesa za kulipia elimu kunaweza kuonekana ya kwamba kunakulemea, lakini pindi tu unapopata habari mwafaka, ni rahisi kufanya.

Jiulize maswali kadhaa ndipo uanze:

  • Je unataka watoto wako wapate elimu bora iwezekanavyo?

  • Je umeshawahi kuwa na ndoto ya kurudi shuleni?

  • Ikiwa wewe ama mtu katika familia yako ataamua kuendeleza elimu yao,je utamsaidia kulipia ada ya mafundisho na gharama zingine?

Ikiwa ulijibu ndio kwa lolote la haya maswali,unahitaji mkakati ili uanze kuhifadhi fedha.Katika hii sehemu utajifunza kuhusu njia mbili za kuhifadhi fedha kwa ajili ya elimu yako ama ya watoto wako.

0
No votes yet
Your rating: None