Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Benki

ATM

Unaweza fikiria kwamba hauhitaji akaunti ya benki, lakini kuwa na akaunti ya benki ama kujiunga na Shirika la Akiiba na Mikopo kuna faida zifuatazo: 

 1. Unajijengea historia ya fedha na rekodi ya matumizi bora ya benki.
 2. Wanakupa sehemu ya kuweka hazina ya pesa yako kwa urahisi.
 3. Unaunda uhusiano mzuri na benki yako ili baadaye uweze kuomba pesa za kununua rasilmali kama gari, nyumba au za kujiendeleza kimasomo.
 4. Kujiunga na SACCO inakuwezesha kujua vile pesa zako zinavyowekwa na unakuwa mmilikaji wa pesa zako. 
Je?
 • Unaweka pesa zako kibetini, mfukoni au kabatini hadi utakapozihitaji?
 • Unaomba pesa kutoka kwa wakopeshaji wadogo?
 • Haulipi bili au deni kwa sababu huna muda wa kwenda kulipa?
 • Unatuma pesa kwa marafiki na majamaa kupitia huduma ya posta au huduma nyingine ya kutuma pesa? 
Ukijibu ndiyo katika baadhi ya maswali hayo basi una uwezo wa kukimu pesa zako vyema. Kwa hivyo:- 
 • Fungua akaunti katika benki. Zunguka kwenye benki kadhaa upate itakayokufaa.
 • Hakikisha kuwa hundi ya mshahara wako imewekwa kwenye benki au SACCO. Waajiri wengi hupendelea kuwalipa waajiriwa moja kwa moja katika akaunti zoa.
 • Weka pesa kwa akaunti hadi utakapo zihitaji.
 • Tembelea benki au SACCO kutoa pesa au utumie ATM au kadi ya kutolea pesa.
 • Lipa bili zako ukitumia hundi au benki ya Intaneti
0
No votes yet
Your rating: None