Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Majonzi na huzuni baada ya kujifungua

Hii ni hali gani? 
Baada ya kupata mtoto kina mama wengi huathirika. Mwili hupitia mabadiliko mengi ya kupanda na kushuka kwa kiwango cha homoni. Wao huhisi majonzi huzuni na hawapati usingizi wa kutosha. Ni hali ya kawaida kuogopa, kuona umeshindwa, kuwa na hisia za huzuni/furaha kwa siku chache baada ya kujifungua. Hata hivyo mama wengine huhisi vibaya sana baada ya kujifungua. Hali hii husababisha kuumia kwa majuma au miezi iwapo hatatibiwa mara moja.
 
Ni nini baadhi ya dalili zake? 
Unahitaji kukaguliwa na daktari ndipo atambue iwapo una huzuni na majonzi ya baada ya kujifungua. Wewe au rafiki yako mnaweza kugundua dalili za kuashiria hali hii. Tajiriba ya kila mwanamke ni ya kipekee. Hivyo basi usijilinganishe na mtu mwingine.
 • Kukosa furaha, kujiona bure na kuhisi kuwa huwezi kufanikiwa katika jambo lolote.
 • Uchovu, kuhisi bure, kuhuzunika ama kuwa na kilio tele.
 • Kuchanganyikiwa na kuwa na wasiwasi.
 • Uwoga wa kumuumiza mtoto
 • Uwoga wa kuwa peke yako ama kwenda nje kutembea
 • Kukosa hamu ya kufanya mambo ya kawaida ya kushirikiana
 • Kukosa kulala au kulala sana
 • Kuishiwa na nguvu
 • Kushindwa kujitunza (kujinadhifisha)
 • Kushindwa kutafakali vizuri ama kufanya maamuzi
 • Kuyaepuka majukumu yako yote na kukataa kuyashughulikia
 • Kuwa na woga wa kukataliwa na mpenzi wako.
 • Fikra za kumuumiza mtoto au wewe mwenyewe.
 
Unautibuje?
Muite daktari wako mara moja tu unapoona hizi dalili na unapitia mapwito ya mabadiliko ya kimaisha kama vile talaka, kutengana, kazi mpya, kuhama ama kufiwa na mtu unayempenda sana. Muone daktari wako iwapo huoni nafuu baada ya majuma mawili au ukianza kuwa na mawazo ya kijitia kitanzi ama kumjeruhi mtoto wako. Daktari anaweza kukupa matibabu na akusaidie kupata mshauri yanayo kufaa.
 
Marafiki na jamaa pia wanaweza kuwa wa manufaa kwako. Unaweza kuhitaji mtu wa kukutunzia mtoto wako huku nawe ukiwa na muda wa kujitunza. Usiogope kuitisha msaada wa kutunziwa mtoto ama kupata mtu wa kukufanyia kazi za nyumbani kwa kupika, kufua na kununua chakula.

0
No votes yet
Your rating: None

Excellent article. Very interesting to read. I really love to read such a nice article. Thanks! keep rocking.
cheap usb flash drives

»