Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kutuma Pesa kwa Jamii na Marafiki Nchini Kenya

Kutuma pesa kwa familia na marafiki kupitia posta sio salama.  Inafaa utumie huduma ya utumaji pesa. Zipo njia mbili za kutuma pesa; kupitia benki au kupitia kampuni za utumaji pesa. 

Benki
 
Kama wewe na yule unayemtumia pesa mna akaunti za benki, unaweza kutuma pesa kwa urahisi pale benki yako inaweza kuhamisha pesa kutoka kwa akaunti yako na kuweka kwa yule unayemtumia.. Benki kawaida hutoza ada sawa kwa kutuma kiasi chochote. Benki nyingi zinaweza kutuma pesa hadi nchi za nje. Shida iliyopo ni kuwa benki huchukua muda wa siku 2 hadi 5 kabla pesa zimfikie unayemtumia.
 
Kampuni za utumaji pesa
 
Njia hii ni ya haraka ya kutuma pesa kuliko benki lakini huwa ghali. Waulize marafiki zako na watu wa familia kuhusu huduma ya kutumia pesa waitumiayo na ujaribu ile ya ada ya chini.
 
Waweza kutuma pesa nchini au ng'ambo ukitumia kampuni kama vile: Safaricom M-Pesa, Western Union na Money Gram.

 

0
No votes yet
Your rating: None

Thanks for sharing the info, keep up the good work going.... I really enjoyed exploring your site. good resource...
cheap usb flash drives

»