Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Mbinu ya kupikia lishe bora

Ikiwa umekuwa na fikira za kubadilisha mtindo mbaya wa kula, basi jifunze kuhusu lishe bora nyumbani ambayo ndiyo sehemu ya kuzingatia kwanza. Hata kama wewe si mpishi hodari, huna budi kujua mbinu bora za kutayarisha vyakula ili kupata virutubishi mwilini. Kwa sababu ukila chakula kilichopikwa na mtu mwingine kama vile hotelini, kwa kweli huwezi kujua kilicho kwenye sahani.
 
Kupika lishe bora siyo tu muhimu kwa kulinda umbo lako, mbali ni muhimu kwa watu wenye matatizo ya kiafya kama vile, wale wenye ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu na ‘cardiovascular disease” na lazima watumie vyakula vyenye ‘cholesterol’ kidogo na sodiamu kidogo ili kuwa na afya bora
 
Basi epukana na mbinu ya kukaanga. Zingatia mbinu zifuatazo za kupika lishe bora ili kuwa na afya nzuri
Kuoka au mbinu ya kuoka chakula.
 
Vyakula vya baharini, batamzinga, kuku, nofu isiyokuwa na mafuta yote hupendeza sana yakipikwa kwenye joko. Tia kwenye bunguu ya kuoka mkate kisha uweke jokoni kwa muda uliopendekezwa kupika, kisha utakuwa umemaliza. Kama ni lazima, tumia mafuta kidogo kupaka kwenye sehemu ya chini ya bunguu (sahani)
 
Kuchoma
Unapotaka kuchoma chakula au kutumia mbinu hii, weka chakula kwenye waya ya kuchomea nyama iliyo juu ya kaa la joto. Kwa vyakula vidogo kama vile mboga iliyokatwa tumia ‘long handled grill basket’, itakayozuia vipande vya mboga kuanguka. Ikiwa unabanika ndani ya chumba weka chakula kwenye ‘rack’ chini ya kaa la moto. Mbinu zote mbili huacha mafuta kudondoka kutoka kwa chakula.
 
Kukaanga
Ikiwa ni lazima ukaange chakula, mbinu bora ni kuchukua kikaangiio kikubwa kilicho na mafuta kidogo kisha utie vipande vidogo vya nyama nofu au kuku na mboga unayopenda. Koroga ili iive vizuri na iwe chakula bora au lishe bora.
 
Kupika au kulainisha chakula kwa mvuke
Mbinu hii hutumia mvuke kutoka kwa maji yaliyochemka
Jaza mtungi kwa inchi moja ya maji, kisha uingize kung’uto, wacha maji ichemke kisha utie mboga halafu ufunike mtungi kwa kifuniko. Pika hadi mboga ilainike.
Mbinu ya kupika chakula kwa kukaanga kwa mafuta kidogo
Mbinu ya kupika chakula kwa kukaanga kwa mafuta kidogo ni sawa na mbinu ya kukaanga, ambayo huivisha chakula kwa haraka. Mbinu hii inahitaji kutia mafuta kidogo kwenye kikaango chini ya joto wastani. Ongeza kuku, nyama ama mboga kwenye kikaango kwa kuzingatia kuwa kuna nafasi ya kutosha kwenye kikaango inayotosha kupika chakula.
 
Tumia aina nyigine ya mafuta badala ya mafuta iliyoloa. Kama maelezo ya upishi yahitaji maziwa, baadhi ya matunda. Tumia mafuta kama vile mafuta ya zeituni. Badala ya mafuta ya kawaida. Badala ya krimu kali tumia jibini au chizi iliyotengenezwa kutoka kwa maziwa machunda. Jaribu na mimea ya msimu kuongeza ladha badala ya chumvi.

1.5
Average: 1.5 (2 votes)
Your rating: None