Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kulipia Bima ya afya

Bima ya afya ni muhimu kwa sababu inaweza kukulipia ada ya hospitali ikiwa hauna pesa.Unaweza kuchagua kati ya bima ya afya ya umma ama ile ya kibafsi. Bima ya afya ya umma nchini Kenya inatolewa na National Hospital Insurance Fund-NHIF ilhali ile ya kibinafsi inatolewa na kampuni za kibinafsi za bima ya matibabu au huwa ni mojawapo ya bima zinazotolewa na kampuni kubwa za bima. Bima ya umma inatolewa kwa Wakenya wote na inashughulikia shida zote za kiafya. Kampuni zinazotoa bima ya kibinafsi ya afya hubagua baadhi ya magonjwa, hutoza ada za juu na zingine haziwashughulikii walio na Ukimwi, ugonjwa wa Sukari au  huwashughuliki watu waloathirika na Virusi vinavyo sababisha Ukimwi/Ukimwi, Kisukari ama magonjwa mengine sugu.Kabla ya kujiunga na bima yoyote ya kibinafsi ya afya unafaa kuhakikisha umeelewa vyema huduma wanazozitoa.Jifunze jinsi unaweza kujiunga na NHIF.

National Hospital Insurance Fund-NHIF
Hii ni bima ya matibabu ya umma inayotolewa kwa wananchi wa Kenya na watu wanaowategemea(mme au mke na watoto).NHIF humsimamia mgonjwa aliyelazwa hospitalini na pia kwa kiwango fulani husimamia kesi za upasuaji katika baadhi ya hospitali hizi.Ili kufuzu;lazima uwe mwanachama utoe mchango  kila mwezi.Ni wazi kwa walioajiriwa na wasio na ajira.Kuna matawi 23 ya NHIF nchini kote na kwa kila hospitali ya wilaya utapata mahali pa kuhudumiwa.Mchango wa watu wailioajoriwa hukatwa na muajiri na kupeanwa kwenye hazina.Watu wa jua kali wanaweza kulipa moja kwa nmoja kwa NHIF Ksh 160 kila mwezi.Yeyote mwenye kipato cha Ksh 1000 ama zaidi amestahiki.
 
Manufaa ya kujiunga na NHIF
  • Humsimamia mgonjwa aliyelazwa hospitalini kiwango cha hadi Ksh 396,000 kila mwaka kwa mwanachama,mme au mke wake na watoto.
  • Huduma ya matibabu kwenye baadhi ya hospitali kote nchini.
  • NHIF hushirikiana na wahudumu wa afya zaidi ya 4000 wanaotambulika na serikali,wa kibinafsi na wa misheni waliosambaa kote nchini.
  • NHIF hurejeshea mwanachama gharama yote aliyotumia hospitalini kulingana na maafikiano.
  • Humsimamia mama anapoenda kujifungua.
  • NHIF haibagui ugonjwa wowote.
Jinsi ya kudai malipo ya hospitalini
Hospitali inaweza wasilisha madai moja kwa moja kwa NSSF baada ya mchangiaji amwetoka hospitalini.Ikiwa hakuna swali lolote kwa madai,NHIF hulipa kabla ya siku 14.Ikiwa mwanachama angependelea kulipa maja kwa moja kwa hospitali,anaweza kuanza madai kwa NHIF ili arejeshelewe pesa zake.
 
Hospitali zinazotambulikana na NHIF
NHIF imezigawa hospitali inazozitambua katika makundi 3:
  • Kundi A-hospitali za Serikali. Wanachama hufurahia huduma zote na  za uzazi na matibabu ya magonjwa ukiongezea upasuaji.Kwa hivyo,kama wewe ni mwanachama,haulipi chochote unapolazwa.
  • Kundi B-Hospitali za Kibinafsi na za Misheni. Wanachama hupata huduma zote lakini ikiwa unahitaji kupasuliwa, mwanachama hujilipia huduma hii.
  • Kundi C-Hospitali za kibinafsi.NHIF hulipia tu manufaa maalum ya kila siku na mwanachama hujilipia kila kitu kingine.
0
No votes yet
Your rating: None