Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kumuona Daktari: Orodha ya unachohitaji kujua

Itakuwamiujiza ikiwa madaktari watawahudumia kila mgonjwa, kwa kuchunguza historia yao ya afya na jamii zao, wakiuliza maswali ya kujenga uhusiano kama:Wahitaji msaada gain kutoka kwa daktari? Je waweza kuzungumzia kuhusu historia ya afya yako bila uoga? Mbona ulimuacha au hukwenda kumuona daktari wako wa mwisho? Ukweli: Wagonjwa ni wengi na muda ni haba na madaktari lazima wafanye kazi kwa madhubuti, ufasaha na haraka.

Kwa hivyo, labda uwe ni miongoni mwa matajiri walio na uwezo wa kuwasiliana na wauguzi kwa simu(ni ndoto nzuri), lazima ujiandae kukutana na daktari ukifahamu vyema unachotarajia na kufatilia kana kwamba afya yako inakitegemea.

Kabla hujamuona daktari
Ni vyema kufahamu unavyojihisi na uhakikishe unaweza kuelezea mambo muhimu yanayokusumbua kabla ya kumuona.Uweze kuelezea dalili za maradhi na lini yalikuanza.Ikiwa huwezi kujieleza vizuri, ziandike au andamana na rafiki unayemthamini au jamaa yako ili akusaidie.

Hapa kuna baadhi ya vitu vichache ambavyo unatarajia daktari kuuliza, jitayarishe kwa miadi naye kwa kuweza kujibu.

Ufahamu:

  • Majina ya madawa, miti shamba na vitamini unayotumia.
  • Uwe na historia ya afya ya jamaa yako, pamoja na historia ya shinikizo ya damu, kisukari, ugonjwa wa moyo, saratani na magonjwa mengine.
  • Eleza hali yako ya afya zamani na sasa, dalili au upasuaji wowote uliofanyiwa.
  • Eleza kwa kina ikiwa umewahi kulazwa kwa vyumba vya dharura, lini, wapi, kwa nini na jinsi ulivyofatilia na muuguzi wako wa kawaida.
  • Eleza majina, anwani na simu za madaktari walio kutibu zamani na wale wanaokutibu sasa.
  • Eleza kwa kina mzio wowote ulionao kwa madawa, chanjo, mazingara pamoja na pumu, ukurutu na kadhalika.
  • Elezea kuhusu pombe, sigara na madawa yoyote yasiyotoka kwa mtaalamu au hospitalini.
  • Toa habari kuhusu bima yako.
1.9
Average: 1.9 (10 votes)
Your rating: None

Kwa Bw. Daudi,
Ikiwa ungetaka kujua zaidi kuhusu uvimbe katika sehemu za siri bonyeza kiunganishi kifuatacho http://kenya.thebeehive.org/content/146/634 Lakini jambo la MUHIMU ni kwamba unapoona dalili ya uvimbe au unahisi kitu kisicho cha kawaida katika sehemu za siri, inatakikana umuone daktari mara moja.

Asante.

»

uvimbe sehemu za siri na namna ya kujilinda na kutibu.

»