Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Utunzi wa mama kabla ya kuzaa

Huu ni utunzi ambao hutolewa kwa mama wakati wa uja uzito ili kuhakikisha ya kwamba mama anabakia kuwa mwenye afya na anajifungua mtoto mwenye afya.Hujumuisha mambo yafuatayo:
 • Ukadiriaji wa hatari zinazoweza kumkumba 
 • Ukadiriaji unaondelea wa ustawi wa kijuzi 
 • Ukadiriaji unaoendelea wa utata
 • Elimu kuhusu usumbufu wa kawaida wakati wa uja uzito,hali ya hisia (ukijumuisha huzuni wa baada ya kujifungua),vikao vya darasa kuhusu kabla ya kujifungua.
 • Majadiliano kuhusu kujifungua na jinsi ya kujifungua
Kujipatia matibabu
Historia ya uvutaji sigara, unywaji wa pombe na matumizi ya madawa inafaa kutathminiwa. Pia wanawake wanashauriwa kutojitibu kabla ya kuangalia kwanza usalama wao na wa mtoto aliyetumboni.  Ni bora kutaja kwamba vitamini na tiba za kutumia mitishamba zinafaa kupunguzwa wakati wa uja uzito. Kwa mfano,  matumizi ya zaidi ya vidonge viwili vya Vitamini A kila siku kunaweza kusababisha dosari za kuzaliwa kwa mtoto atakayezaliwa.  
 
Mlo
Ushauri kuhusu mlo unafaa kutilia mkazo mlo kamili na vyakula tofauti tofauti ukisisitizia kabohaidreti changamani na protini, pamoja na kiasi cha kutosha cha foliate (miligramu 0.5), chuma (miligramu 15) ,kalshiamu (miligramu 1200) na maji (lita 2-3) kila siku.
 
Tembelea kituo cha afya ya mama wajawazito
Tembelea ktuo cha afya ya mama wajawazito kila mwezi  katika kipindi cha kwanza cha wiki 28, baadaye nenda baada ya kila wiki mbili mpaka wiki ya 36. Kutoka hapa nenda kila wiki  mpaka siku ya kuzaa. Kila wakati unapotembelea kituo cha afya, hali ya afya yako na ya mtoto wako inaangaliwa.

Usumbufu wa kawaida wakati wa ujauzito

 • Ongezeko la kutaka kwenda haja ndogo ni kawaida lakini linafaa kufanyiwa uchunguzi kwani 8% ya wanawake waja wazito watakuwa na maambukizo katika eneo wanalotumia katika haja ndogo ambayo hayaonyeshi dalili.
 • Uvimbe katika kifundo cha mguu unaweza kuhusishwa na kushinikiza kwa mishipa itwayo inferior vena cava. Ikiwa kuvimba hakuambati na shinikizo la damu, tiba huwa kupumzisha miguu ikiwa imewekelewa juu kama vile ya kiti au kwa kutumia vyakula kama Celery au Vitamin B6 ambazo kwa kawaida huondoa maji mwili kupitia kukojoa mara nyingi.   
 • Kufura kwa mishipa kwa sababu zizo hizo na kupata nafuu baada ya kufuungiwa kunaweza kuwa kwa kushtua. Pindi tu inapotambulika, matumizi ya mapema ya stokingi za kushikilia ni jambo la busara; ilhali matumizi ya mda mfupi ya kiinua fupanyonga na vipande vya barafu vinaweza kumaliza dalili hizi za kufura kwa mishipa katikaa tupu.
 • Kiungulia husababishwana kupwa kwa tumbo na umio pamoja na ongezeko la shinikizo la tumbo.Ushauri wa mkao na mlo pamoja na matumizi ya vimaliza asidi humaliza mengi ya haya, lakini mpinzani wa H2 (kitengo cha B katika uja uzito) anahitajika mara moja moja.
 • Uyabisi wa tumbo (kuwa na gesi kwa tumbo) unaweza kutokea mapema lakini angalau husababishwa na homoni lakini unaweza kuzidishwa na ongezeko la yaliyomo kwenye fupanyonga.Ongezeko la ukubwa wa mishipa na kushinikizwa kwa mishipa katika fupanyonga kunaweza kusababisha kufura kwa mishipa. Wanawake wanapaswa kushauriwa kuongeza matumizi yao ya uoevu na ufumwele na ikiwa dawa za kuharisha zinahitajika zinapaswa ziwe za aina ya ufumwele k.m Metamucil ama Fybogel.
 • Kuumwa na sehemu ya chini ya mgongo ni jambo la kawaida kwa sababu ya kubadilika kwa hali ya mkao. 
 • Kuoza kwa meno na magonjwa ya tishu zinazozunguka meno huongezeka wakati wa uja uzito na unafaa kushughulikiwa na dakitari mapema. 
 • Mabadiliko katika ngozi yanajumuisha madoa ya hudhurungi kwenye ngoziambayo hutoweka baada ya ujauzito. 
 • Mikwaruzo hutokea katika 17% ya wanawake waja wazito. La kuvutia ni ya kwamba 50% ya wanawake wenye ugonjwa wa ngozi huonyesha dalili za kupata afueni wakati wa uja uzito. Ikiwa hakuna kipele, zingatia ukosefu wa chuma ama hali inayoweza kuwa hatari ya kusimama ama kupunguza kasi ya mtiririko wa nyongo wakati wa uja uzito. Dawa za kuzuia mzio zinaweza kuwa za manufaa.
 • Alama zinazobakia kwenye ngozi ya tumbo, mapaja, makalio ilinyooka baada ya uja uzito ikiwa ukuaji umekuwa wa haraka. Ukavu na kujikunakuna kunaweza kutulizwa na mafuta ya mboga ama krimu ya Vitamini E na kutotumia sabuni.

 

2.375
Average: 2.4 (8 votes)
Your rating: None

tips about pregnancy that are quite useful for obat keputihan gatal and jas hujan axio yogya

»

Positive site, where did u come up with the information on this posting? I'm pleased I discovered it though, ill be checking back soon to find out what additional posts you include.
usb 3 flash drive

»