Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kujifungua/uchungu wa kujifungua

Katika wiki zako za mwisho za mimba, mji wako mimba (uterus) utaanza kurudiana kujikunja. Hii huita Braxton-Hicks Contractions (au uchungu wa kujifungua usio wa kweli) na huwa wa kawaida. Kwa sana hili hutokea ukikaribia kujifungua, ni vigumu kwa wanawake wengi kujua kama ni uchungu wa kweli au usio wa kweli.
 
Ongea na daktari wako kama:
  • Unapata mikunjano hii (contractions) baada ya sekunde 30-70, inaendelea bila kukoma na inaendelea kuwa mikali zaidi.
  • Unaumwa na sehemu ya chini ya mgongo na uchungu huu haukomi.
  • Hata kama uchungu wa kujifungua huwa tofauti, huwa na awamu tatu kwa kawaida.

Awamu ya kwanza
Hiki kipindi ndicho hukoa sana. Huanza wakati mlago wa uzazi huanza kuwa mwembamba na kufunguka. Ule ulio na damu huanza kutoka ukeni (‘show’). Karibu na mwisho wa awamu hii mikunjano huu huana mikali zaidi na huchukua muda mrefu pia.
 
Awamu ya pili
Mlango wa uzazi hufunguka kabisa na mtoto anahitaji usaidizi ili atoke. Utahitajika kumsukuma mtoto ili atoke wakati wa mkunjano hadi mtoto atakapotoka. Awamu hii inaweza kukaa hata masaa mawili au zaidi hasa kama ni mara yako ya kwanza.
 
Awamu ya tatu
Baada ya kujifungua utaendelea kupata mikunjano ili kito ‘placenta’. Mikunjano hii huja ikikaribiana zaidi kuliko ile ya kabla hujajifungra lakini haina uchungu kama ya awali. Awamu hii inaweza kukaa kwa dakika chache na kukaa kwa dakika 15-20.
 
Baada ya kujifungua utachungwa kwa uangalifu mwingi ili kuhakikisha hauna matatizo yoyote. Joto la mwili wako, mpigo wa moyo, kupumua na mwendo wa damu zitachunguzwa mara kwa mara. Katika wakati huu, unaweza kuanza kumjua mtoto wako. Kama ulikuwa umepanga kumnyonyesha mwanao unaweza kuanza wakati huu.

3.105265
Average: 3.1 (19 votes)
Your rating: None

i was just browsing along and came upon your blog. just wanted to say good blog and this article really helped me.
halogen light bulbs

»