Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Baada ya kujifungua

Wakati huu, baada ya kujifungua, huitwa ‘post partum period’. Huu ni wakati utakapokuwa na mabadiliko mengi sana maishani kwa sabababu una mtoto wa kutunza. Ni vizuri kufuata maagizo yale daktari wako atakupa na ujitunze wewe na mtoto wako.
Haya ni baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kuufanya wakati huu rahisi.
 • Pata pumziko la kutosha- Hili ni jambo moja muhimu sana unafaa kuzingatia siku za kwanza baada ya kujifungua. Jilaze chini ili kupata usingizi kila wakati mwanao anapolala.
 • Usifanye kazi nyingi punde sana- Uliza usaidizi kutoka kwa marafiki na familia ili wakusaidia kionya, kupika na shughuli zingine za kila siku.
 • Fanya mazoezi rahisi rahisi- Unaweza taka moili wako urudie umbo/ukubwa wake kabla ya kupata mimba. Yaweza kuchukua muda mrefu ili misuli ya tumbo iliyokuwa imekunjuka kurudia hali yake ya awali, lakini mazoezi rahisi yanaweza saidia. Anza kufanya mazoezi taratibu na kasha kuongezea mazoezi polepole. Kama unanyonyesha, hakikisha umenwona daktari wako kabla ya kuanza zoezi lolote.
 • Tambua kwamba mwili wako bado unabadilika- Mwili wako utaendelea kubadilika jinsi unavyoendelea kupona tangu kujifungua. Siku za kwanza utakosa starehe. Tumbo la mama huanza kujikuja na linaporudia ukubwa wake wa kawaida, matiti yaki yatajaa na kuuma,na mguu yako inaweza kuanza kufura. Pia utapata majimaji yakitoka ukeni yaitwayo ‘lochia’. Huwa damu na tabaka la tumbo la uzazi. Pia haya huwa ya kawaida na hukoma baada na ya siku kadhaa.
 • Kula chakula kilicho na afya na unywi maji mengi. Kama unanyonyesha ongea na daktari wako kuhusu chakula unachotaka kula.
 
Kama utaona mabadilika yafuatayo, mwite daktari wako haraka iwezekanavyo:
 • Joto ya juu ya 38oc
 • Uchefuchefu na kutapika
 • Uchugu unapokonjoa, kuchomeka unaponjoa au haja ya kukonjoa kwa ghafla.
 • Damu ya hedhi nyingi kuliko kawaida na huendelea siku nyingi kuliko 1on2.
 • Uchugu, kufura au miguu yako kuwa miororo
 • Uchugu kwa kifua na homa
 • Matiti moto na nyororo
 • Uchugu kati ya uke na huendelea kuwa mkali.

3.4
Average: 3.4 (5 votes)
Your rating: None

This article was written by a real thinking writer. I agree many of the with the solid points made by the writer. I’ll be back.
halogen light bulbs

»