Wiki moja baada ya kujifungua unaweza kuanza kupata mabadiliko ya tabia (furaha na hasira) yanayo sababishwa na mabadiliko ya ‘Hormone’, uchovu na mahangaiko kwa sababu ya mtoto wako kukufanya ukasirike. Haya ni matukio ya kawaida na hutoweka baada ya wiki chache.
Kwa matukio mengine, wanawake huhuzunika hata wanashindwa kujitunza na kutunza watoto wao. Haya majonzi huitwa ‘Post natal’ au ‘Post partum depression’. Kama kukasirika huku kutaendelea kwa zaidi ya wiki mbili au kama una yafuatayo, hakikisha umemwona daktari wako:
- Haupati usingizi au unakasirika haraka
- Una huzuni, umekasirika na unakaa ukilialia
- Hauna nguvu
- Unaumwa na kichwa na kifua unapumua harakaharaka, moyo wako unapiga kwa kasi au unasikia kama moyo unaruka midundo Fulani.
- Haukuli au unakula sana
- Haufikirii vizuri, haukubuki mambo au hauwezi kufanya uchaguzi
- Hauna hamu tena ya uliokuea unapenda kama kufanya mapenzi
- Haupati shughuli na mtoto wako
- Unajisikia kama hauna maana tena na unajihurumia
- Unaogopa utamuumiza mtoto au utajiumiza