Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kumuona Daktari

Kuchagua daktari wa mtoto

Unatakiwa kumchagua daktari wa mtoto wako kama ungali mja mzito miezi 3 kabla ya kujifungua. Waulize marafiki, jamaa au daktari wako. Waweza kupata matibabu ya bure kwa watoto wachanga kutoka kwa hospitali za mikowa au kliniki za jamii, kwa malipo ya chini katika hospitali za serikali. Mchaguwe daktari uliye na imani naye aliyemzuri mwenye kuelewa na maono tofauti na pana.
 
Uchunguzi wa mara kwa mara
 
Mtoto wako anahitaji kuonekana na daktari kila mara ili akuwe kwa raha na afya. Watoto wana ratiba yao ya kupelekwa kwa daktari.
 
 • Kati ya masaa 24 baada ya kuzaliwa
 • Siku 2-4 baada ya kuzaliwa ikiwa mtoto atapelekwa nyumbani chini ya masaa 48 baada ya kuzaliwa.
 • Wiki 2-4
 • Miezi 2
 • Miezi 4
 • Miezi 6
 • Miezi 9
 • Miezi 12.
 Unachotarajia kwa uchunguzi wa kila mara
 
Kila uchunguzi daktari hutizama urefu wa motto,uzito,na kichwa cha mtoto ili kufahamu jinsi motto anvyokuwa.Daktari pia atachunguza macho ya mtoto, masikio, mapafu, moyo, mdomo, sehemu nyeti na tumbo. Katika muda wa mwaka mmoja mtoto wako antakiwa kukaa,kugaagaa na kujivuta mwenyewe hadi asimame.
 
Chanjo:
 
Mtoto kupelekwa kupata chanjo ni muhimu, inapendekezwa watoto wapate chanjo hizi kuzuia maradhi kuhatarisha maisha yao.
 
 • Homa ya manjano B (Hepatitis)
 • Dondakoo, Pepopunda na Pertussis – Diptheria, Tetanus, Pertussis (DTP)
 • Polio
 • Surua, matumbwitumbwi, Rubella – Measles, Mumps, Rubella (MMR)
 • Haemophilus influenzae type B (HIB)
 • Varicella, Tetewanga – Chicken Pox
0
No votes yet
Your rating: None