Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ukingo wa Uzazi

Ukingo wa uzazi ni nini? 

Huu ni wakati wanawake hufikia kikomo cha kupata damu ya hedhi na kutoweza kuzaa. Muda huu huanza kutoka umri wa miaka 40. Hali hii yaweza kuanza polepole au kwa ghafla. Ukingo wa uzazi huathiri kila mwanamke tofauti.

Kuna aina za upasuliwaji unaoweza kuleta hali hii. Kwa mfano, katika 'hysterectomy' tumbo la uzazi likiiondolewa, itasimamisha hedhi zako . Pia ovari zote mbili zikitolewa, hali hii huja mara moja licha ya umri wako.
 
Dalili za ukingo wa uzazi
 • Siku za hedhi kubadilika badilika
 • Kuumwa na viungo
 • Hali ya kusahau mambo
 • Mabadiliko ya hisia za kimapenzi
 • Kutokwa jasho kwa wingi
 • Kuumwa na kichwa
 • Kukojoa kila mara
 • Kuamka mapema kuliko kawaida
 • Hali ya kukauka ukeni
 • Kubadilika kwa hisia
 • Kukosa usingizi
 • Kutokwa jasho usiku

Utapambana vipi na dalili hizi?

 • Matibabu ya hormone, kama vile; vidonge na krimu ya kuweka ukeni
 • Fanyisha viungo vyote mazoezi, fanya mazoezi ya kuinua uzito na kunyorosha misuli.
 • Kula kwa wingi matunda na mboga na vyakula visivyo na mafuta nyingi. Pia kula vyakula vilivyo tengenezwa na soya.
 • Wanawake wengi pia hufaidika na ushauri wa mtaalamu wa afya ya akili wakati huu wa maisha yao.

 

 

0
No votes yet
Your rating: None

hi was just seeing if you minded a comment. i like your website and the thme you picked is super. I will be back.
heated ice cream scoop

»