Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Maambukizi ya Kuvu – Yeast Infection

Wanawake wengi watapata maambukizi haya katika maisha yao. Maambukizi haya huwasha, ni chungu lakini ni rahisi kutibu. Walio na ugonjwa wa Sukari huambukizwa haraka kwa sababu ya sukari nyingi katika damu yao. Pia kwa wanao ugua Ukimwi. Daktari atakupa madawa ya kutibu.

Nini dalili za maambukizi ya kuvu? 
 • Kuwashwa ndani na nje ya uke.
 • Golegole nzito yenye gamu kutoka kwenye uke
 • Uchungu au hali ya kuchomeka unapokojoa au kushiriki ngono
 • Ngozi iliyogeuka nyekundu sehemu ya uke
 • Golegole inayotoka katika uke yenye harufu mbaya
 • Ishara kujitokeza juma moja kabla ya kwenda hedhi. 
Unatibu vipi maambukizi haya.
 
Kama umewahi kuambukizwa basi unaweza kununua kirimu ya anti-fungal na ujipake, ikiwa hujawahi kuambukizwa basi muone daktari akushauri.
 
Utazuia vipi maambukizi ya ukungu 
 • Wacha kutumia dawa za kuua bakteria - antibiotics ikiwa si lazima
 • Kunywa maziwa mala - yorghurt kupiga vita bakteria
 • Usivae chupi zinazokubana sana. Vaa chupi za nyuzi za pamba na zisizikubane
 • Osha mikono na iwe imekauka kila wakati
 • Jaribu usitumie marashi, poda na sabuni za marashi kuosha sehemu nyeti 
 • Osha sehemu nyeti kila mara na uhakikishe umekausha vizuri
 • Jaribu kuimarisha kiwango cha sukari katika damu yako
 • Tumia kondomu na wacha kushiriki ngono ukitumia midomo.

 

0
No votes yet
Your rating: None

You make so many great points here that I read your article a couple of times. Your views are in accordance with my own for the most part. This is great content for your readers.
heated ice cream scoop

»