Vizuizi vya Ghafla (Emergency Contraception)
Hii hutumika wakati mwanamke amefanya mapenzi kiholela kupitia kwa uke (vaginal sex) ili kumzuia kupata mimba. Inaweza kutumika pia kama njia za kizuizi zilizokuwa zimetumika hazikufaulu. Hufaa sana kama itachukuliwa kabla ya masaa 72 kutoka wakati wa mapenzi. Huhusisha kunywa dawa mbili za ‘Hormone’ zikiachana kwa masaa 12. Hizi dawa vidonge hufaa kwa asilimia 75-89 kuzuia mimba.
Njia nyingine ya kizuizi cha ghafla ni kuwekwa ‘copper T IUD’ kwenye tumbo la uzazi kabla siku 7 hazijaisha kutoka wakati wa mapenzi (ngono). Hii njia hufaa asilimia 99.9 kuzuia mimba na inaweza kutolewa wakati wa muezi huo mwingine. Kama tayari ushaishika mimba njia hizi hazitakusaidia. Hii njia za ghafia hazifai kutumika kama desturi.
Povu na utando,
Povu na utando au vidonge vilivyo na kemikali ya kuua mbegu (manii) – spermicide huwekwe ndani ya uke si zaidi ya saa moja kabla ya kufanya mapenzi. Huwa zinafanya kazi kwa kuua manii. Huachwa papo hapo kwa masaa 6-8 baada ya kufanya mapenzi. Kemikali hizi (spermicides) zingine huwa na Nonoxynol-9 ambayo kukulinda kutokana na kisonono na Chlamydia. Nonoxynol-9 hatakulinda kutokana na ukimwi. Kemikali hizi (spermicides) hufaa kwa asilimia 74 kukulinda kushia mimba.
IUD (Intrauterine Device)
Hiki ni kifaa cha plastiki au shaba kilicho na umbo la ‘T’ na huwekwa kwenye mji wa mimba/tumbo la uzazi (uterus) ili kuzuia manii kulifikia yai. Hukaa kwa muda wa miezi kadha hadi miaka 10. Hiki kufaa husaidia asilimia 98-99 kuzuia mimba. Kinapowekwa, huanza kazi yake papo hapo. Unaweza kupata kiharusi siku chache baada ya kuwekwa IUD. Kati ya mwezi wa 3 na 6 unaweza kutoa damu kidogo juu zaidi ya damu ya hedhi. Pia mwezi wako/wakati wako wa hedhi utakosa kubainika. Wanawake wengine hutoa damu kwa wingi.