Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Jinsi ya kutunza Uwezo wako wa kusikia

Jinsi unavyozidi kuzeeka ndivyo uwezo wako wa kusikia unaharibika.Watu waliofanya kazi kuliko na kelele nyingi kwa muda mrefu kama wajenzi, wafanyikazi viwandani, wanaweza kupata kuharibikiwa zaidi. Mara nyingine upungufu wa uwezo wa kusikia husababishwa na maradhi au dawa.
 
Dalili za kukuonyesha unapoteza uwezo wa kusikia:
  • Utawataka watu kurudia walichosema mara kwa mara.
  • Unapata matatizo kufuata mazungumzo ya watu zaidi ya wawili.
  • Unafungulia runinga au redio sauti ya juu wengine watataka ipinguzwe.
  • Unapata wakati mgumu kuelewa watu unapoongea kwa simu.
 
Kama unafikiria/unajua una matatizo ya kusikia:
  • Mwone daktari
  • Pata ukaguzi/uchunguzi wa uwezo wako wa kusikia.
  • Taka kujua kama unahitaji mtaalamu wa masikio au kifaa cha kukusaidia kusikia.
0
No votes yet
Your rating: None