Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Magonjwa ya Zinaa

Aina za magonjwa ya zinaa, ishara na dalili zake
 
STDs ni magonjwa ya zinaa, pia hujulikana kama maambukizo ya zinaa (STIs). Kwa maneno mengine ni maaambukizo yanayopitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia ngono. STIs husababishwa na bakteria na virusi.
 
STIs za kawaida ambazo husababishwa na bakteria zinajumuisha; Kaswende, Kisonono na Klamidia. Magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na virusi yanajumuisha; Ukimwi na Genital Herpes. Genital Herpes ni ugonjwa wa malengelenge ya neva ngozini unaoathiri viungo vya uzazi.
 
Unaweza kuathirika na magonjwa ya zinaa zaidi ya moja kwa wakati mmoja na mara kwa mara ikiwa umepatikana kuwa na ambukizo moja, unahitajika kupimwa ikiwa una magonjwa mengine ya zinaa ukijumuisha HIV.
 
Ni muhimu kufahamu ya kwamba mtu aliye na magonjwa ya zinaa yuko katika hatari kubwa ya kuambukizwa na HIV, kwa sababu STI hufungulia virusi njia ya kuingia mwilini. Ikiwa umepatikana na STI, unafaa kupimwa ikiwa una HIV. Wale ambao wameathirika na STI na HIV pia husambaza HIV kwa haraka kwa watu wengine. Kwa hivyo ni muhimu watibiwe haraka iwezekanavyo.

 

1
Average: 1 (2 votes)
Your rating: None

Impressive web site, Distinguished feedback that I can tackle. Im moving forward and may apply to my current job as a pet sitter, which is very enjoyable, but I need to additional expand. Regards.
halogen light bulbs

»