Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Umuhimu wa elimu kwa waschana

Elimu ya watoto wa kike ni moja ya njia bora za kupunguza umaskini katika mataifa yanayostawi. Manufaa ya elimu yao yanaweza kuonekana kwa watu binafsi, familia zao na kwa jamii yote. Manufaa haya yanajumuisha:
Kupunguza idadi ya watoto ambayo wanawake hujifungua;

  • Kupunguza viwango vya vifo vya watoto wakembe na watoto wadogo;
  • Hupunguza viwango vya vifo vya akina mama;
  • Hulinda dhidi ya maambukizo ya HIV/UKIMWI;
  • Huongeza idadi ya wanawake wenye kazi na mapato ya juu;
  • Mapato haya hudumu kwa vizazi vingi.

Elimu ya wasichana inaweza kuwa na faida ya kuchelewesha ndoa na uja uzito kwa wasichana wadogo. Badala ya msichana kuolewa kabla ahitimishe umri wa miaka 20 na mara kwa mara aathirike na dhuluma kutoka kwa mme wake, kuna uwezekano wa wasichana ambao huenda katika shule za msingi na shule za upili kuwa na usemi mkubwa kuhusu yule mtu watakayeolewa naye.Wanawake ambao wameenda shule wanaweza kutumia kwa njia inaayofaa mbinu za upangaji uzazi na kwa hivyo huwa na watoto wachache wenye afya. Msichana na mwanamke aliyeelimika atakuwa amejifunza kuhusu HIV/UKIMWI na atafahamu njia nyingi tofauti za kujilinda dhidi ya gonjwa hili. Kila mwaka wa kuelimika humsaidia msichana kufanya maamuzi bora, yake na ya familia yake.

Wanawake wanaoenda shuleni kwa kawaida huwa na familia zenye afya.Kuna uwezekano kwa wanawake hawa kutafuta usaidizi wa matibabu kutoka kwenye kliniki ama madaktari. Kwa sababu wanaweza kusoma,wanawake wenye elimu wanaweza kuelewa kwa kinaganaga maagizo ya daktari na kutafuta usaidizi ikiwa unahitajika.Wanawake hawa pia wanaweza kusoma vitambulisho vya lishe na kutolea familia zao lishe yenye afya ambayo hukuza ukuaji na ina kiwango kidogo cha cholesterol. Elimu pia huwafunza watoto wadogo umuhimu wa kuweka miili yao katika hali usafi na umuhimu wa kuweka nyumba katika hali ya usafi na salama.

Kwa sababu familia zao huwa zenye afya, mama vilevile huwa na mwenye afya. Pia hupunguza uwezekano wa kuwa mama mchanga kwa sababu alikaa shuleni na atakuwa na uja uzito uliopangwa vizuri na ambao haudhuru afya yake. Elimu ni ya kustaajabisha: Benki ya Dunia ilibainisha ya kwamba kila mwaka wa elimu huzuia vifo 2 vya uzazi katika wanawake 1000 kila mwaka!

Kuwapeleka watoto wako wa kike shuleni kunaweza kuwa changamoto kwa mfuko wako na usalama wake. Unaweza kuwalinda kupitia usaidizi wako na kujihusisha katika elimu yao.Hilo litapunguza kwa kiasi kikubwa usumbufu wa walimu na wanafunzi ambao watahisi wana wasiwasi nao. Endelea kusoma kiunganishi ili ujionee jinsi thamani ya gharama kwa mfuko wako itakuwa hivi sasa na katika mda unaofuata.
(World Bank)

 

 

 

0
No votes yet
Your rating: None

Here you can HACK FACBOOK online and get password to somebody else fb account access easily online for free.

»