Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Chaguo la shule

Hoja ya kwanza unahitaji kuchagua kama utampeleka mtoto wako shule ya chekechea akiwa bado mdogo. Kwa wengi wao hii si hoja – Kwa wazazi wanaofanya kazi lazima wawapeleke watoto wao katika kituo cha kulea watoto wachanga halafu shule za chekechea. Kwa bahati mbaya hii huweza kuwa ghali na hakuna usaidizi wa serikali kwa kiwango hiki, lakini ukiuliza utapata kuna vituo vya kulea watoto wachanga na shule za chekechea zinazodhaminiwa na makanisa na mashirika ya kijamii katika maeneo yako, wanaopeana huduma nzuri kwa bei nafuu.

Shule nyingi za umma zinaanza na shule ya malezi ili motto aweze kukubaliwa katika Standard 1, ingawaje, si lazima umpeleke mtoto wako Standard 1 kwa shule alipoanzia. Shule nyingi ulaya ni bora kwa nyanja nyingi kuliko zingine – nyingine zinaweza kuwa na vifaa bora vya michezo ama vitengo bora vya usanii, kwa hivyo wazazi lazima wawapeleke watoto wao kwa shule ya malezi ya ile shule inanawiri kwa Nyanja wangetaka mwanao asomee. Wazazi wengi wanachagua shule zilizoko karibu nao. Shule nyingi zinawapendekeza watoto wanaishi karibu.

Shule binafsi zinaweza kuwa ghali, wanapeana huduma nyingi sanasana kulingana na vifaa. Ukiwa huna budi basi fanya utafiti wa shule kwa upate ile itakayo mfaa mtoto wako.

0
No votes yet
Your rating: None