Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Tayarisha mtoto wako kwenda shule

beautiful school girl

Kutayarisha mtoto kwenda shule huanza mapema. Unaweza msaidia mtoto wako kwa kuwa makini katika vipengele vifuatavyo: 

Akili ya kufahamu kinachoendelea: Mfunze mtoto wako mtaa wenu na nambari ya nyumba yenu, nambari ya simu, jina lake kamili na siku ya kuzaliwa. Mtoto wako akikuuliza maswali kuhusu malimwengu, yaani kuhusu mambo yanayo mzingira, jaribu kujibu vyema unavyoweza au umpeleke maktabani kutafuta majibu.

Kujitegemea: Mtoto wako lazima ajue kuvaa na kuvua nguo na kutumia zipu, vifungo, vifungo vya bubanisha na vinginevyo. Lazima awe ameanza kujifunza kufunga kanda za viatu. Watoto katika shule ya awali (nursery) wanahitaji kujua kutoa makamasi na kujiendea msalani peke yao.

Kuweka nembo (label) vitu vyao: Nguo zote za mtoto wako, kalamu na vinginevyo vinahitaji kuwekwa alama. Muonyeshe mtoto wako pale alama ilipo na mfunze kuitambua – hii itakuwa rahisi kwake kupata na kuhifadhi vitu vyake shuleni. Mfunze mtoto wako kuwa na jukumu la vitu vyake na hivyo utaweza kuhifadhi pesa zako na pia kumfunza maarifa bora ya maisha ya kuwajibika.

Lisha mtoto wako vyema: Watoto wanafanya vyema shuleni kama wamepata kiamsha kinywa kizuri na wamebeba chakula cha mchana chenye afya. Kipande cha mkate wa sandiwichi na tunda ni tosha kwa mtoto anayekuja nyumbani kwa chakula cha mchana. Kama wanabaki shuleni ama hawapatiwi chakula cha mchana, muongeze mkate na njugu – karoti na mboga. Wazazi wengi huona rahisi kupatia mtoto pesa anunue paketi ya chipsi na soda baridi. Lakini sandiwichi na kujaza chupa ya jusi halisi ya matunda ni bora zaidi kwa mtoto wako.

5
Average: 5 (1 vote)
Your rating: None