Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Elimu Spesheli (wanafunzi walio na shida ya masomo)


Elimu spesheli ni elimu iliyo juu na zaidi ya madarasa ya kawaida ambayo inasaidia mtoto mwenye ‘matatizo ya kusoma’ matatizo haya yanaweza kuwa ulemavu wa kimaumbile au ulemavu wa akili.

Mtoto mwenye ulemavu wa kimaumbile anaweza kuwa na matatizo ya kuona ama kusikia au hawezi kutembea. Mtoto mwenye ulemavu wa akili anaweza kuwa na ugonjwa wa autistic, bipolar au dyslexic, au hali nyingine zinazomfanya kusoma kwa shida.

Nani anahitaji elimu ya kitengo maalum au spesheli?
Elimu ya kitengo maalum kawaida inapatiwa watoto wenye hali kama:

  • Ugonjwa wa akili kama Downs Syndrome na Autism na mengineo
  • Upungufu wa makini - “Attention Deficit Disorders (ADHD)”
  • Matatizo ya kusikia, kuona na kuongea.
     

Ni zipi baadhi ya dalili za ulemavu wa kusoma?
Utafanya nini kudhania mtoto wako ana ulemavu wa masomo?
Na yafanyikeje ikiwa mtoto wako ana ulemavu wa masomo?