Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Utafanya nini kama unadhani mtoto wako ana ulemavu wa masomo?

Ukidhani mtoto wako anaulemavu wa masomo, kwanza ongea na mwalimu wake kujua kama wanaona matatizo darasani. Wataweza kukushauri hatua nyingine. Ikiwa dalili hazijionyeshi wazi, na si kawaida iwe hivi, utaelekezwa kwa mtaalam wa saikologia ya elimu kwa majaribio. Kwa kawaida watoto wenye ADHD, dyslexia, matatizo ya misuli minene na misuli sawa wanaelekezwa kwa muuguzi wa kuwafanyisha mazoezi. (Occupation Therapist) Inaweza kubadilika ikiwa shida ya mtoto wako ina husika na shida ya kuona ama kusikia, ambapo utaelekezwa kwa daktari wa macho na daktari wa masikio.

Matibabu haya yanahitaji pesa, ingawaje wengine wanaweza lipiwa na huduma ya matibabu. Pata ushauri kutoka kwa shule ya mtoto wako na daktari wa akili wa shule (counsellor) kama kunae mmoja kabla hujakimbilia ratiba ya matibabu ambayo inaweza kutokuwa sahihi kwa mtoto wako.

0
No votes yet
Your rating: None