Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Msaada wa masomo na nafasi za kusoma

Msaada wa masomo wa Mafunzo ya utalaam wa viwanda na biashara (TIVET)

Msaada huu  wa masomo unatolewa na wizara ya elimu ya juu, sayansi na teknolojia. Unalenga kuwawezesha vijana maskini na mayatima waliopoteza wazazi kutokana na Ukimwi, wanaoishi sehemu za ukame na vitongoji duni vilevile wanaoishi sehemu za mashambani ambazo hazina sehemu za mafunzo ya utaalam wa viwanda na biashara. Mradi huu pia huhamasisha ushirikiano wa akina dada na wasiojiweza.
 
Mpango wa msaada wa masomo unalenga:
  • Mayatima waliopoteza wazazi kutokana na Ukimwi ambao wangetaka kupata mafunzo ya utaalam wa viwanda, dini na biashara.
  • Vijana wenye mahitaji maalum.
  • Vijana kutoka nyumba maskini katika sehemu kame na mitaa ya mabanda mijini.
  • Vijana wanawake ambao wangependa kufanya  kozi za utalaam ambazo hutawaliwa na wanaume. 

Jinsi ya kuomba msaada wa masomo

Wizara hutangaza msaada wa masomo katika vyombo vya habari.Mtu mwenye haja anaweza pata fomu ya maombi katika makao makuu ya wizara ama katika ofisi za elimu ya wilaya.Fomu pia zinaweza kutolewa kwenye Intanetiukitumia anwani ifuatao www.scienceandtechnology.go.ke.Fomu hizi ni bure.
Ili uhitimu ndio utume maombi,ni lazima uwe umejiandikisha na mafunzo ya utalaam wa viwanda,dini na biashara (uwe mwanafunzi anayeendelea) ama ni lazima uwe na barua ya kusajiliwa kwa mojawapo wa shule hizi.

 

 

 

 

1.88889
Average: 1.9 (9 votes)
Your rating: None