Watoto wengi hushikwa na chawa angalau mara moja. Chawa ni wadudu wanaoishi kwenye nywele. Hutaga mayai sehemu ya chini ya nywele.Chawa haisababishwi na uchafu, ila ni sehemu, hali ya kawaida utotoni. Hupatikana sana shuleni na nasari na ni rahisi sana kuenea kwa vikundi vya watoto.
Namna ya kuzuia chawa
- Angalia kichwa na nywele ya mtoto wako kama pana dalili ya kuwa na chawa. Usimruhusu mtoto wako kutumia vichana vya watoto wengine au kuvaa kofia zao.
- Ikiwa mtoto wako ana chawa, hakikisha kuwa wengine nyumbani wametibiwa.
- Usikaribiane na mtu aliye na chawa
Jinsi ya kujua kama mtoto wako ana chawa
- Je, kichwa chake kinawasha?
- Ana alama nyekundu kichwani na shingo?
- Je, ana vipele shingoni?
- Je, wewe houna chawa kwa kitanda na nguo za mtoto wako?
Ikiwa majibu yako ni ndiyo, angalia kichwa chake kwa makini kama kuna chawa au mayai. Chawa ni wadudu wadogo wa rangi ya njano-jivu wenye miguu sita. Unaweza kuwaona shingoni au karibu na maskio. Mayai yao hufanana na mchanga mweupe ukiwa kwenye nywele.
Mtoto wako ikiwa ana chawa
- Mtibu nyumbani haraka iwezekanavyo. Fua kila kitu kinachotumiwa na mtoto wako (blanketi, shuka, nguo, taulo, vichana) kwa maji moto iliyo na sabuni iliyo na dawa ya kuua viini.
- Tumia sabuni kutoka duka la dawa ya kuua chawa. Tumia kichana kinachokuja na dawa kuondoa chawa waliokufa. Dawa ya chawa ni hatari isipotumiwa vilivyo. Fuata maagizo ya jinsi ya kuitumia.
- Ikiwa hutaki kutumia kemikali, tia kichwa cha mtoto wako kwa mafuta ya Zeituni (Olive oil) Chawa ‘wanazama’ kwa mafuta ya mzeituni. Ukitumia kichana kilicho na meno madodo, chana nywele kwa uangalifu ukuondoa mayai ya chawa.
- Pia unaweza kuosha kichwa chake kwa kutumia mchanganyiko wa maji na siki (vinegar). Chana vizuri ili kuondoa chawa. Wacha mtoto wako akae nyumbai mpaka atibiwe.
- Ukishindwa kuwatoa chawa, basi muone daktari.
- Wajulishe walimu shuleni kuhusu hali ya mtoto wako. Katika shule zingine yaenda uitishwe kibali kutoka kwa daktari kuhakikisha kwamba chawa zimeisha.