Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Mfumo wa Mawasiliano

Man on Computer

“Mfumo wa mawasiliano” Hii ni kauli inayozua dhana ya kuzungumza na watu huku ukiwataarifu kuwa unatafuta kazi. Kila mtu ana mawasiliano; inastahili utambue ni kina nani walio katika upande wako na ni jinsi gani utawapata ili kukusaidia kupata kazi.

Namna ya Kuwasiliana:

Hatua ya kuanza: Tengeneza orodha ya mawasiliano:
Tengeneza orodha ya kila rafiki na watu wa familia yako walio na uzoefu wa kazi. Nakili nambari zao za rununu (simu) na anwani zao.

Hatua ya pili: iipe orodha yako kipaumbele:
Tambua watu wanaoweza kukusaidia kwenye orodha yako. Kwa mfano, unaweza kuhitaji kuzungumza kwanza kabisa na mtu fulani aliye na kazi katika mahali unapotaka kufanya kazi ama rafiki anayewafahamu watu wengi.

Hatua ya tatu: Anza kuwasiliana:
Unapompigia fulani simu, unaweza kusema hivi;“Habari John, huyu ni Tracy kutoka kanisani.Nimehitimu katika mafunzo ya taaluma ya tarakilishi /kompyuta na sasa nimeanza kutafuta kazi. Najua unafanya na kampuni hiyo, na nilidhani kwamba unaweza kuwa na wazo nyeti la jinsi nitakavyoanza.

  • KIDOKEZO: Onyesha/dhihirisha umahiri au ubingwa wako na maarifa.
    Na kama watu unaowasiliana nao hawajui kazi uliyo na ujuzi kwayo, hawatakusaidia sana.

Hatua ya nne; Usiwe vivo hivo bila kuwa na jina mtu mwengine wa kumpigia simu:

Ingawa watu unaowapigia simu hawana habari kuhusu kazi, huenda labda wanawajua watu wawili au watatu ambao unaweza kuwapigia kwa msaada. Na unapompigia mtu uliyependekezewa, unaweza kusema hivi:

“Hallo, Bi. Smith? Nimeelekezwa kwako na John Davis. Tunashiriki Kanisa moja. Nilimtajia John kuwa natafuta kazi katika nyanja ya kompyuta/Tarakilishi na akaongeza kusema kuwa una ufahamu na kwamba unaweza kunielekeza kwenye mkondo /upande mzuri”

Hatua ya tano: Fuatilia ukitumia wasifukazi:
Tengeneza nakala za wasifukazi wako na umtumie kila mmoja aliye katika mawasiliano yako ambaye anaweza kukusaidia (ukiwahusisha watu wapya uliowaweka katika mawasiliano yako). Ambatanisha barua yasmi ya utangulizi ukiwashukuru kwa mapokezi yao mazuri kwako huku ukiwakumbusha aina za kazi unazozitafuta.

2
Average: 2 (1 vote)
Your rating: None