Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

  • Unafaa uzingatie nini unapochagua shule?

Unafaa uzingatie nini unapochagua shule?

Kenyan student

Kuna mengi ya kuzingatia unapochagua shule bora kwa mtoto wako. Ukiwa unawahamisha kwa shule nyengine au ukiwachagulia shule ili wakaanze, ni uamuzi mkubwa. Unajua chaguo gani bora?


Saizi ya darasa / shule:
Baadhi ya wanafunzi wanafanya vyema. Nambari ya wanafunzi kwa kila darasa inaweza kutofautisha vile mtoto wako ataweza kusoma. Ingawaje shule za serikali huwa na madarasa makubwa, lakini ukifanya utafiti utapata baadhi zina madarasa madogo. Shule binafsi kawaida zina madarasa madogo.

Saizi ya shule: Baadhi ya wanafunzi wanafanya vyema katika shule kubwa ambapo kuna wanafunzi wengi wakucheza nao na kuchagua madarasa wayapendayo. Wengine hupenda shule ndogo hakuna madarasa mengi na kuna uhusiano wa karibu na wanafunzi na walimu. Ingawaje walimu wengi ni watu waliojitolea na wenye bidii na wanaweza kufanya kila wawezavyo kumpa makini kila motto kama anavyohitaji, shule ikiwa kubwa inakuwa vigumu.

Maeneo: Familia nyingi huchagua shule zilizoko karibu nao. Lazima uzingatie usalama
wa mtoto wako katika safari yake yakwenda na kurudi shule, vifaa vilivyoko katika maeneo vilevile kama mktaba, dimbwi la kuogelea na kadhalika.

Mgawanyiko: Baadhi ya wazazi hupenda shule zinazozingatia tabaka na mgawanyiko wa tamaduni zao. Unaweza kutazama nje ya jamii yako ukitaka mtoto wako awe na uzoefu wa shule za tamaduni tofauti.

Karo za shule: Shule zote za uma zinatoza karo kama ilivyopendekezwa na serikali, kama haunauwezo wakulipa karo wanakukubalia mtoto wako – hakuna mtoto anaenyimwa elimu ya msingi nchini Kenya. Uliza shule zilizo vijijini kuhusu karo “Malipo yanayofichwa” (Kama vile vitabu, kalamu, chokaa na vyenginevyo) na kupunguziwa malipo ya karo kwa watoto wadogo. Shule binafsi wanalipisha karo ya juu na hawapunguzi malipo, lakini wanapatiana basari kwa wanafunzi wanaostahiki.
 

0
No votes yet
Your rating: None