Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Dumisha mtazamo halisi (chanya)

Njia bora kusaidia watoto wako kufanya vyema shuleni ni kuonyesha kwamba shule na kazi za ziada ni mhimu kwako na familia nzima.

Ndio, kuna njia nyingine nyingi kuwaonyesha watoto wako unajali. Haya hapa baadhi ya mawaidha ya kusaidia.

  • Wewe ni mwalimu wa kwanza na muhimu kwa mtoto wako. Unawajua watoto wako zaidi kuliko mtu mwingine, na bila shaka unawajali kuliko mtu mwengine, jihusishe katika elimu yao kutoka hatua ya kwanza – kutoka kwa uzaidi wa kazi nyumbani hadi kongamano la mzazi na mwalimu.
  • Uhusiano wa karibu utamuondolea kuwa na matatizo shuleni: Watoto wanahitaji usiaidizi wa kufanya maamuzi kuhusu shule, uhusiano, kufanya maamuzi kuhusu shule, uhusiano, kufanya kazi na kukua. Hii inaweza kuwa rahisi ikiwa watoto wako wanaweza kukueleza chochote.
  • Kuwa msikilizaji mzuri: Watoto wadogo wanapenda kuzungumza kuhusu wakati wao shuleni, hivyo basi pata wakati wa kuongea na kusikiliza kila siku. Kadri watoto wanapokua, sanasana katika shule za upili, huweza, wasipende kuongea sana.
  • Kuwa na subira: Fikiria mbinu za kujiingiza katika maisha ya watoto wako.
  • Mpongeze mtoto wako: Unahitaji kuwa mcheshi kwa watoto wako. Waambie watoto wako unajivunia wakiwa wanastahili. Hakikisha unawapongeza watoto wakijitahidi.
  • Peana usaidizi wako: Saidia watoto wako kujifunza jedwali la hesabu za mara au waache wakusomee makala moja wapo. Ikiwa watoto wako wanashida shuleni wasaidie kutoka katika shida.

Mukiwa na uhusiano mzuri na wakuaminika na watoto wako itawasaidia kufaulu shuleni. Hata kama haukufurahia kuwa shuleni, unaweza kuwasaidia watoto wako kufaulu. Imani yako na usaidizi wako unaleta tofauti kubwa.

 

 

 

0
No votes yet
Your rating: None